NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA
HALMASHAURI
kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma imeazimia kuwa Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 bado ina nguvu,hivyo
hakuna ulazima wa kuichokonoa kwa kutafuta katiba mpya hasa ile
pendekezwa.
Maazimio hayo
yamepitishwa leo jijini hapa katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM
Mkoani Dodoma,ambapo pamoja na mambo mengine pia kimempongeza Rais wa
Tanzania Mh,Samia Suluhu Hassan kwa kushika nafasi ya juu ya uongozi
nchini.
Aidha akiongea
katika kikao hicho Mwenyekiti wa CCM Mkoa Godwin Mkanwa amesema katika
siku 37 alizokaa madarakani Rais Samia Suluhu Hassan nchi imetulia na
mambo yote yanaenda kama yalivyo pangwa na miradi ya maendeleo
inaendelea kutekelezwa.
"Ni
maoni ya Halmashauri kuu kuwa Si nchi zote zingeweza kupita na kuwa
salama katika mazingira magumu ya kuondokewa na kiongozi mkuu wa nchi
na nchi kubaki salama kama ilivyokuwa kwa nchi yetu hivyo basi
Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa wa Dodoma inaona Katiba yetu ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 bado ina nguvu na imefanikiwa
kutupitisha salama katika kipindi kigumu ni kipimo cha kwanza na cha
wazi kwa Katiba yetu"amesema Mkanwa.
Hata
hivyo amesema Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa wa Dodoma imeona Katiba
hiyo bado inafaa na hakuna ulazima wa kuibadilisha kwa kutafuta Katiba
mpya wakati iliyopo bado inafaa.
"Mathalani
katiba pendekezwa kwenye jambo hili ilikuwa inasema Rais akifariki
zikipita siku 90 uitishwe uchaguzi wa kujaza nafasi hivyo halmashauri
kuu ya Mkoa wa Dodoma inaona kama katiba pendekezwa ingekuwa ndio Katiba
inayotumika isingetutoa salama mpaka tukawa kama hivi tulivyo
leo"amesema Mkanwa.
Sambamba
na hayo ametoa wito kwa watanzania wote kwa umoja kuunga mkono Serikali
ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan na
kuwataka wafanye kazi kwa bidii na kulipa kodi ili nchi iweze
kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo na kuboresha utoaji wa huduma za
kijamii.
Maazimio hayo yanajiri wakati ambapo chama cha mapinduzi kikitarajia kufanya mkutano wa chama hicho April 30.
No comments:
Post a Comment