Na Said Hauni, Lindi
UONGOZI wa Kijiji cha Mchichili Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi,
umetaja changamoto zinazodaiwa kukwamisha usimamizi na utunzaji wa
Misitu ni wafugaji na wakulima kuvamia maeneo ya hifadhi kufanya
shughuli zao za kibinaadamu.
Afisa Mtendaji wa Kijiji
hich,Husna Kijazi,ameyaeleza hayo katika mahojiano maalum na timu ya
waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari ilipotembelea Kijijini hapo
kuona shughuli za kimaendeleo zinazofanywa na Jamii.
Kijazi
amesema changamoto nyingi inazoikabili hifadhi ya Misitu iliyopo katika
maeneo ya Kijiji hicho,ni pamoja na uvamizi wa mifugo unaofanywa na
wafugaji,wakulima na uvunaji haramu wa mazao yanayotokana na Misitu na
kukosekana kwa Soko la uhakika kwa Jamii ya Miji isiyofahamika.
Kijazi
alisema iwapo serikali itakipa kijiji hicho kipaumbele cha
kuvuna,kununua na kuuza mazao yanayotokana na Misitu iliyopo kwenye
hifadhi ya vijiji kutekeleza Miradi mbalimbali ya Maendeleo,kutasaidia
kukuza soko la ndani na kupunguza tatizo hilo kwa jamii.
Pia,ameshauri
ni vizuri kamati za Mali asili zikapewa Mafunzo ya mgambo ili kusaidia
uvamizi wa uvunaji haramu wa rasilimali misitu na wafugaji kuendelea
kuvamia bila kufuata taratibu zilizopo kutoka mamlaka husika.
Mtendaji
huyo wa kijiji amesema licha ya uwepo wa changamoto hizo,yapo baadhi ya
mafanikio yaliyopatikana kutokana na utekelezaji wa mpango wa usimamizi
shirikishi wa Misitu ya hifadhi za vijiji,ikiwemo ujenzi wa Ofisi
Serikali za vijiji,Zahanati,Nyumba za kuishi walimu,vyumba vya madarasa,
maabara,vyoo na utengenezaji wa madawati na ununuzi wa Trekta la
kijiji.
No comments:
Post a Comment