HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 09, 2021

Waziri Mhagama atoa maagizo 22


 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira Vijana na wenye Ulemevu na Uwekezaji, Jenista Mhagama.
 
 

NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira Vijana na wenye Ulemevu na Uwekezaji Jenista Mhagama ametoa maagizo 22 kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuanza kwa mfumo wa kusaidia utendaji kazi ndani ya Ofisi katika kitengo cha TEHAMA  uwe umekamilika ifikapo Aprili mwaka huu.

Mheshimiwa Mhagama ametoa maagizo hayo leo jijini Dodoma katika kikao maalum wakati alipokuwa akizungumza na Wakuu wa idara mbalimbali wakiwemo wakurugenzi.

Amesema kuwa kuwepo kwa mfumo huo utasaidia kuondoa tatizo la rushwa katika suala la vibali vya ajira kwa wageni kutokana nna kucheleweshwa kwa vibali hivyo.


Aidha amesema hatasita kumchukulia hatua mtendaji ambaye atashindwa kutekeleza majukumu yake kutokana na uzembe .

"Hii iko wazi kwani hata Rais wetu Samia Suluhu Hassan tayari ameshajipambanua kuhusu suala zima la utendaji kazi na kuacha kufanya kazi kwa mazoea," amesema.

Sanjari na hilo amegiza Taazizi zote za Sheria kusimamaia sheria za kazi ili kusikiliza malalamiko ikiwa ni pamoja na kuyapatia ufumbuzi.


Katika hatua nyingine Waziri huyo amemuagiza Katibu Mkuu kuliangalia kwa kina watumishi ambao wanasifa na wamekaimu nafasi  kwa muda mrefu wawapandishe vyeo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tickson Nzunda ameahidi kuyafanyia kazi yote aliyoagizwa na kwamba hatawavumilia watendaji wazembe.


No comments:

Post a Comment

Pages