Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo ambae pia ni Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar Othman Masoud Othman amewataka wanachama wa chama hicho kushikamana kwa pamoja ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa.
Kauli hiyo alitoa huko shangani Mkokotoni Wilaya ya Kaskazini A Unguja wakati kikao cha kutambulishwa kwake kwa viongozi na wafuasi wa chama hicho.
Alisema umoja na mshikamano uliomo ndani ya chama hicho ndio uliokipa nguvu na heshima ndani ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
“Wazee wetu walisema umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu na ambapo mshikamano huo ndio uliopelekea uimara wa chama ”
Alieleza kuwa mshikamno uliopo ndani ya Act Wazalendo imepelekea kuzuia migogoro na malumbano ndani ya chama hicho.
“Kwa sababu ya mshikamano wetu tumekuwa hatuyumbi katika kudai haki pamoja na mamlaka ya Zanzibar ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania ” alisema Othman.
Alifahamisha kua wanzanzibar na watanzania wengi wanaingia katika chama cha Act wazalendo kwa kile alichokitaja kuvutiwa na mashirikiano, Juhudi na dhamira njema.
Aliwataka wafuasi wa chama hicho kutoichezea dhana waliyonayo kwani ndio njia pekee yakufikia kule waliko kusudia kuongoza Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Aidha alisema ili kuyaenzi aliyoyaacha kiongozi wetu marehemu maalim Seif Sharif Hamad ni kuendeleza umoja na mshikamano alioupigania kwa miaka mingi uhai wake na historia ya nchi ya Zanzibar.
Mjumbe huyo wa kamati kuu alisema kuwa mshikamano umewajenga ari wanachama na kuweza kushindana na watu waliokuwa na nguvu ya dola na kueleza kuwa chama hicho kinajivunia rasilimali watu.
Sambamba na hayo alisema chama cha Act wazalendo kimeingia katika serikali ya umoja wa kitaifa GNU kwa ya kuleta umoja na mshikamano bila ya kujali madhila waliyopitia kutokana na nguvu kubwa walizotumia watawala.
“Tunalopigania tuendeshe nchi yetu kistarabu pasina mtu yoyote kupata madhara wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi kwani tuna haki ya kuishi kwa amani katika nchi yetu.”alisema.
Mapema makamo mwenye kiti wa chama hicho Juma Duni Haji akimtambulisha kiongozi huyo alimtaka kuyasimamia yote aliyoyaacha maalim Seif ambayo yana maslahi Zanzibar pamoja na chama kwa ujumla.
“leo nakutambulisha kwa viongozi wa mikoa ninachokuomba sasa usikae nyuma tuanze kazi ya kujenga chama na kupigania haki za wazanzibar” alisema Babu Juma.
Alisema kuwa Mjumbe huyo awali alikuwa msaidizi Mkubwa wa maalim Seif sharif wakati wa Uhai wake hasa kwa upande wa sheria.
Kwa upande wake katibu wa habar na uenezi wa chama hicho Salum Abdalla Bimani alisema nchi hii inataka demokrasia ya kweli yenye maelewane ili nchi iweze kuneemeka kutokana mashirikiano anamini Zanzibar itarudi kwenye hadhi yake.
“Mshikamano na umoja wetu ndani ya Zanzibar utapelekea kupata viongozi ambao watachaguliwa na wananchi kwa maana kwamba Yule aliyeshinda katika uchaguzi apewe haki yake”alisema Bimani.
Akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa Mkoa wa Kaskazini A Kichama Ali Angali Ali kwa niaba ya wafuasi wa chama hicho alisema wakotayari kumpatia mashirikiano yale ambayo yatampatia nguvu katika kutekeleza majukumu yake kichama na kiserikali.
No comments:
Post a Comment