HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 04, 2021

NMB yaandaa kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu Zanzibar


Mapokezi ya Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Lela Mohamed Mussa (kushoto) aliyefungua kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Lela Mohamed Mussa akifungua kongamano la wanafunzi wa vuo vikuu lililofanyika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein, Tunguu Zanzibar mwishoni mwa wiki. 

Beatrice Mwambije wa NMB (kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri Lela (kulia).
Ofisa wa NMB, Hesbon Mpate (kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Utalii na mambo ya kale, Lela Mohamed Mussa (wa pili kulia).
Picha ya pamoja kati ya Waziri (wa tano kulia) na maofisa wa benki ya NMB baada ya ufunguzi wa kongamano mwishoni mwa wiki.

 

Na Mwandishi Wetu

 

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Leila Muhammed Mussa amewataka wanafunzi wa vyuo vikuu kisiwani humo kuzitumia fursa zinazotolewa na Benki ya NMB ili kujenga msingi mzuri wa kuweza kujiajiri na kuajiriwa pindi wanapomaliza masomo yao.

Aliyasema hayo alipokuwa akifungua kongamano la kusaidia safari ya wanafunzi mbalimbali wa vyuo vikuu katika kufikia malengo yao katika kutafuta fursa za kujiajiri na kuajiriwa pindi wanaomaliza masomo “NMB Career fair”  lililofanyika katika ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein wa chuo kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA mwishoni mwa wiki.

“Wanafunzi wengi wanaohitimu vyuo wanashindwa kuzitumia taaluma zao hivyo kupitia kongamano hili itawasaidia vijana hawa kuzifikia fursa za ajira na kujiongezea ujuzi ambao watautumia katika majukumu yao ya kazi,” alisema Mhe. Leila

Pia amewaomba waandalizi wa kongamano hilo benki ya NMB kuangalia uwezekano wa kuwasaidia wanafunzi wanaomaliza elimu ya sekondari kwani wengi wao wanapomaliza masomo hawajui masomo ya kuchukua ambayo yatawasaidia kukamilisha ndoto zao za baadae.

“Serikali ya awamu ya nane ipo tayari kushirikiana na taasisi mbalimbali zinazolenga kuwasaidia vijana hususani katika mbinu za kuwasaidia kupata ajira ili kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira nchini,” alisema Mhe. Leila.

Naye, Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya NMB, Juma Kimori amesema lengo la kuwakutanisha wanafunzi hao ni kuwapa mbinu mbadala za kutambua fursa za kuweza  kujiajiri na kuajiriwa ambazo watazitumia pindi watapomaliza masomo yao.

Amesema mbali na hilo pia NMB inaunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya 8 chini ya Rais Dkt Mwinyi ambayo imelenga kutengezeza fursa za ajira laki tatu, hivyo kupitia taaluma hiyo itawasaidia vijana kupata ujuzi wa kuzifikia ajira hizo.

Kwa upande wake Rais wa asasi ya vijana ya AIESEC, Michael Chacha amesema asasi yao imekuwa ikiwasaidia vijana mbalimbali kwa kuwajengea uwezo ili kubadilisha mitazamo na fikra zao hivyo wataendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali ili kuona vijana wanasaidiwa na wanaondokana na dhana ya  kusubiri ajira serikalini.

Nao baadhi ya wanafunzi waliopatiwa taaluma katika kongamano hilo la “NMB Career fair” wameipongeza benki ya NMB kwa kuwapatia mbinu ambayo itawasaidia kujiajiri na kuondokana na kusubiri kuajiriwa.

Zaidi ya wanafunzi elfu 1000 kutoka vyuo vikuu mbalimbali vya Zanzibar wameshiriki katika kongamano hilo.

No comments:

Post a Comment

Pages