HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 30, 2026

Rais Samia amteua Dk. Chang'a Mkurugenzi Mkuu TMA

Na Mwandishi Wetu 

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amemteua Dk. Ladislaus Chang'a kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).

Uteuzi wa Dk. Chang'a umetangazwa leo Januari 29,2026 na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Moses Kusiluka kupitia taarifa kwa vyombo vya habari.

Kabla ya uteuzi huo, Dk. Chang'a alikuwa akikaimu nafasi ya Ukurugenzi Mkuu wa TMA, baada ya kustaafu kwa Dk. Agnes Kijazi aliyehudumu nafasi hiyo kwa karibu miaka 20.


No comments:

Post a Comment

Pages