Shirika
la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imeendesha mafunzo ya kuwajengea
uwezo wahariri na waandishi wa habari juu ya shughuli zake na sheria
zinazosimamia sekta ya majini.
Akiwasilisha
mada katika semina hiyo Afisa Uhusiano wa TASAC, bw.Nicholaus
Kinyariri alisema lengo la semina hii ni kuwajengea uelewa na uwezo wa
jinsi ya kuripoti maswala yanayohusu sekta hiyo.
Amebainisha
kuwa TASAC ipo chini ya wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na kwamba
imeanzishwa chini ya kifungu namba 4 cha sheria 14 ya mwaka 2017 ambayo
rasmi ilianza kutumika mwaka 2018.
"TASAC
imeamua kutoa semina hii kutokana na kuwepo uelewa mdogo kwa jamii
kuhusiana na shughuli zake na sheria mbalimbali zinazosimamia sekta ya
majini, " Alisema bw. Nicholaus.
Alisema
TASAC ina majukumu mbalimbali inayotekeleza yakiwemo ya usimamizi na
udhibiti huduma za Bandari na usafiri wa Meli, Biashara ya Meli katika
maeneo husika pamoja na kusimamia maslahi mapana ya bidhaa za kipekee
wanzaopaswa kuzisimamia.
"TASAC pia imepewa jukumu la kusajili vyombo vya majini kuanzia mita nne, vyombo vya Uvuvi na Starehe." Alisema.
Aliongeza
kuwa tangu TASAC kuanzishwa kwake imeweza kupata mafanikio mbalimbali
ikiwemo kuchangia gawio kwa serikali la Sh Bilioni 40, utoaji wa leseni
804 za Uwakala wa meli, kachangia mapato ya serikali pamoja na kuboresha
huduma za usafiri wa majini.
Pia
alibainisha kuwa shirika katika kutimiza majukumu yake wanashirikiana
na wadau wengine wakiwemo mamlaka ya Mapato Tanzania {TRA), Jeshi la
Polisi-kikosi cha Majini, Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) na
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini ( TMA).
Kwa
upande wake Meneja Udhibiti wa huduma za Bandari bw. Julius Mitinje
Alisema shirika hilo linafanya udhibiti katika maeneo ya mwambao wa
bandari za Dar es salaam, Tanga na Mtwara pia kwa upande wa maziwa ni
Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa.
Alisema wamekuwa wakifanya uhakiki wa uzito wa mizigo ndani ya makasha, Bandari kavu na watoa huduma mchanganyiko bandarini.
No comments:
Post a Comment