HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 06, 2021

TIMU YA TAIFA RIADHA KUPIMA VIWANGO TULIA MARATHONI



Kocha wa timu ya Taifa ya riadha, Thomas John akielezea namna timu yake ilivyojiandaa kuelekea mashindao ya riadha ya Tulia Akson Mbeya City Marathoni yatakatofanyika Jumamosi Mei 8/2021 jijini Mbeya.
Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Riadha Tanzania, John Bayo akizingumzia maandalizi ya timu ya Taifa ya Riadha Tanzania.



Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Riadha wakifanya mazoezi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.


 
NA SULEIMAN MSUYA, ARUSHA

WACHEZAJI tisa wa Timu ya Taifa ya Riadha inatarajiwa kushiriki mashindano ya riadha ya Tulia Akson Mbeya City Maradhoni yanayotarajiwa kufanyika  jijini Mbeya Mei 8,2021.

Wachezaji hao tisa ni kati ya 14 waliopo kwenye kambi inayiendelea kwenye Chuo cha Misitu Olmotonyi wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Riadha Tanzania John Bayo, wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii jijini Arusha ambapo timu hiyo iliweka kambi ya mazoezi.

Bayo amesema wameamua kupeleka wachezaji hao tisa ili waweze kutumia mbio hizo kujipima kabla ya kushiriki mashindao ya riadha ya kimataifa ikiwemo Mashindano ya Olimpiki Japani.

Amesema wachezaji wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanaibuka na medani zitakazotolewa.

"Wachezaji wamejiandaa vizuri kushiriki Tulia Maradhoni imani yetu ni wao waibuke kidedea na kujiandaa na mashindano ya kimataifa," amesema.

Bayo amesema wameamua kuweka kambi ya muda mrefu ili kuandaa wakimbiaji wenye uwezo watakao wakilisha nchi vizuri.

Makamu Mwenyekiti huyo alisema shirikisho hilo linakabiliwa na ukata hivyo ameomba wadau kujitokeza ili kusaidia wachezaji.

Kuhusu faida inayopatikana kwa kuandaa marathoni mara kwa mara amesema kwa upande fulani wamenufaika kwa kupata fedha na maandalizi wachezaji.

Kwa upande wake Mwalimu wa Timu ya Taifa ya Marathoni Thomas John amesema vijana wake wamejindaa vizuri kuhakikisha wanaibuka ushindi.

Amesema wiki iliyopita walifanya jaribio ya mbio za uwanjani kwenye mita 100, 200, 500, 800, 1,500 na 5,000 hivyo ni imani yake wakiwa Mbeya wataonesha uwezo wao kwa kuibuka na ushindi.

"Tulia Akson Mbeya City Marathoni itakuwa kipimo sahihi kwa vijana wetu naomba Watanzania wajitokeze Jumamosi kushuhudia vipaji vya kukimbia," amesema.

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Wanaridhia Tanzania, Endrew Boniface amesema wao kama wachezaji wamejiandaa vizuri kutumia Tulia Akson Mbeya City Marathoni kupima viwango.

"Tumejipanga kushiriki mashindano haya kwa nguvu zote kuhakikisha tunaibuka washindi pamoja na changamoto chache amambazo zinatokea," amesema.

Boniface amesema Serikali inapaswa kusaidia wachezaji waliofikia viwango vya olimpiki ya Japani ili waendelee kujiandaa.

Pia amesema serikali inawajibu wa kuandaa wachezaji wengine ili waweze kufikia viwango vinavyohitaji.

Naye Mdau wa Riadha, Juliana Mwamsuva amesema mashindao ya Tulia Akson Mbeya City Marathoni amewataka wanariadha wanaoshiriki kujituma ili kuitangaza Tanzania kimataifa.

"Mchezo huu unalipa iwapo kila mdau ataunga mkono bila kuleta ubaguzi," amesema


Mwisho

Caption

1.Picha No.5
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Riadha wakifanya mazoezi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

2.Picha no.4 Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Riadha Tanzania, John Bayo akizingumzia maandalizi ya timu ya Taifa ya Riadha Tanzania.

3.Picha No.9

No comments:

Post a Comment

Pages