Mkuu mpya wa Wilaya Bagamoyo Zainabu Issa wa kati kati akipokea maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Ramadhani Possi wa kulia wakati wa ziara maalumu kwa ajili ya kutembelea na kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo ambayo inatarajiwa kupitiwa na mbio za Mwenge wa uhuru mwaka 2021 kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Kasilda Mgeni.
VICTOR MASANGU, BAGAMOYO
MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Issa amewaonya vijana na kuwataka kuachana kabisa na vitendo vya matumizi ya madawa ya kulevya ambavyo vimekuwa vikipelekea baadhi ya vijana kupoteza nguvu kazi ya taifa na kuahidi kulivalia njuga suala hilo kwa kuwashirikisha kuwapatia vijana hao fursa mbali mbali zilizopo kwa lengo la kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasikini.
Hayo ameyabainisha wakati ziara maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya kupitia miradi mbali mbali itakayopitiwa na mbio za mwenge wa uhuru wa mwaka 2021 ambapo ilijumuisha viongozi mbali mbali wa serikali ya Wilaya nzima ya Bagamoyo wakiwemo wakurugenzi, wakuu wa idara, pamoja na kamati ya ulinzi na usalama lengo ikiwa ni kujionea mwenendo mzima sambamba na kutoa mapendekezo yao.
Katika ziara hiyo Mkuu huyo alipokuwa katika mradi wa mapambano dhidi ya dawa za kulevya ambao upo katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo aliweza kuwatembelea vijana hao na kuwaasa kuachana kabisa na vitendo hivyo vya matumizi ya madawa ya kulevya na kwamba wanatakiwa kujirekebisha na kujikita zaidi katika kushiriki kikamilifu katika shughuli mbali mbali za uzalishaji mali.
“Mimi kama mkuu wa Wilaya mpya ya Bagamoyo nimekuja hapa kuwatembelea na kujitambulisha kwenu lakini kitu kikubwa ninawaomba sana kubadilika na suala la matumizi ya madawa ya kulevya ni hatari sana kwa afya yenu na kwamba kufanya hivyo kunasababisha madhara makubwa na pia kunapelekea kwa kiasi kikubwa kutpoteza nguvu kazi ya Taifa hivyo ombi langu hili ninawaomba sana mlifanyia kazi vijana wa Bagamoyo ,”alisema Mku huyo.
Aidha amewataka vijana hao ambao hapo awali walikuwa wamejiingia katika matumizi ya madawa ya kulevya kuhakikisha wanazingatia maelekezo yote ambayo wanapatiwa na wataalamu wa afya na kwamba atakuwa nao bega kwa bega katika kuwasaidia kuwainua kiuchumi kupitia fursa mbali mbali amabzo zitakuwa zikijitokeza.
Akiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo aliupongeza uongozi huo kwa kutekeleza agizo la serikali kwa kuweka mfumo mzuri wa ukusanyaji wa mapato na kwamba ana imani kwamba utaweza kusaidia zaidi katika suala zima la kuongeza kipato na kuwataka waendelee na mfumo huo ili kuthibiti wizi la wizi wa fedha .
Kadhalika aliwataka kuhakikisha wanajiwekea utaratibu mzuri hospitalini hapo wa kuhakikisha wanashughulikia chagamoto ya ukosefu wa madawa kwa lengo la kuwawezesha wananchi kupata huduma ya matibabu kwa uhakika.
“Nimeweza kujionea jinsi ya mfumo wa makusanyo ya mapato katika Hospitali hii ya Wilaya ya Bagamoyo na kimsingi ameupongeza uongozi kwa kazi nzuri ambayo ambao wameifanya na kwamba waendelee kujitahidi zaidi katika kuboresha sekta ya afya na kwamba serikali ya awamu ya sita itaendelea kuongeza kasi zaidi katika huduma ya afya,”alisema Mkuu huyo.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo aliwaataka watumishi wa halmashauri zote mbili za Bagamoyo na Chalinze kufanya kazi kwa kuzingatia sharia na taratibu zote na kwamba wasimamie miradi mbali mbali ya maendeleo kwa maslahi ya wanachi na Taifa kwa ujumla.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Kasilda Mgeni ameahidi kuyafanyia kazi yale yote amabyo yameelekezwa na Mkuu wa Wilaya na kubainisha kwamba atashirikiana bega kwa began a watumishi wenzake katika kusikiliza kero na changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.
Nao baadhi ya vijana ambao wameachana na matumizi ya madwa ya kulvya Fasto Fikiri na Shukuru Mohamed wamemshukuru wametoa pongezi zao za dhati kwa Mkuu huyo mpya kwa kwenda kuwatembelea na kuwaasa na madawa ya kulevya na kwamba wameahidi kutojiingiza tena katika matumizi hayo na kutumiza fursa zilizopo katika kuleta mabadiliko chanya ya kiuchumi.
Katika ziara hiyo wajumbe waliweza kutembelea na kukagua zaidi ya miradi 15 ya ikiwemo ujenzi wa restaurant ya msolwa, mapamabano dhidi ya rushwa,ujenzi wa barabara ya round about chalinze, ujenzi wa tanki la maji safi Mboga,ujenzi wa zahanati ya kihangaiko,mapambano dhidi ya ukimwi,shamba la kilimo cha mboga mboga,ujenzi wa chumba cha maabara,ujen zi wa soka la kisasa la samaki,pamoja na mapambano ya madawa ya kulevya.
No comments:
Post a Comment