Msanii wa Kizazi kipya, Ambwene Yessayah, katika akiwa na wachezaji chipukizi wa Simba na Yanga kijijini Mwanzega, Mkuranga.
Picha ya pamoja na msanii AY na Mkuu wa wilaya ya Mkuranga,Philberto Sanga.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya kuuza vifaa vya michezo nchini, Issere Sports imetoa jezi seti mbili za Simba na Yanga na mpira mmoja kwa vijana wanaoshabikia Klabu hizo warshio kijiji cha wasanii wa SHIWATA Mwanzega, Mkuranga.
Akikabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi wa Masoko wa Issere Sports, Abbas Issere alisema anaungana na SHIWATA kukuza vipaji vya vijana wenye mapenzi ya Klabu mbili kubwa nchini kupata vipaji vipya.
Mwenyekiti wa SHIWATA, Deo Kway nguli alisema huo ni mwanzo wa kusimamia kutafuta vipaji katika mchezo wa mpira wa miguu na michezo mingine.
Msanii maarufu wa kizazi kipya nchini Ambwene Yassayah (AY) akizungumza kijijini Mwanzega aliahidi kushirikiana na SHIWATA kuleta hadhi ya wasanii wa SHIWATA kijijini Mwanzega.
AY ambaye amekubali kuwarudisha wanamuziki wenzake kama balozi mpya wa kijiji hicho cha wasanii wa fani mbalimbali alisema hicho kitakuwa kijiji cha mfano nchini
Katika ziara hiyo mwanamuziki AY aliyewawakilisha Joseph Haule (Profesa J),Fareed Kubanda (FED Q),Hamisi Mwinjuma (Mwana FA) alisema kijiji cha wasanii kitawakomboa.
Mkuu wa wilaya ya Mkuranga, Sanga aliahidi kutimiza ahadi kwa kijiji cha wasanii Mwanzega kwa miundombinu ya barabara,Umeme na nani said na Salama.
Mkuu wa wilaya Sanga akizungumzia jezi na mipira kwa vijana wa kijiji cha wasanii alisema michezo ni Afya hivyo anampongeza mwanachama Issere Sports kutoa vifaa hivyo vya michezo.
Mwenyekiti wa SHIWATA, Deo Kway alisema mtandao huo imeanza kutoa maeneo ya wazi yaliyotengwa kwa ajili ya wawekezaji wa sanaa mbalimbali.
Mwenyekiti Deo alisema SHIWATA mbali ya wasanii wanachama kukamilisha ujenzi nyumba zaidi ya 250 pia ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa kuongeza watu 2,000 kwa pamoja baada kukabidhiwa ramani ya ukumbi huo.
No comments:
Post a Comment