Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), alipokuwa
akijibu swali bungeni kuhusu ucheleweshaji wa uteuzi wa Bodi za Taasisi,
bungeni jijini Dodoma.
NA SAIDINA MSANGI, WFM
SERIKALI imesema kuwa siyo
sahihi kuwa na Kanzidata ya Upekuzi
(Benki ya Waliopekuliwa) ili kurahisisha mchakato wa upekuzi kwa kuwa utendaji
na mienendo ya maafisa
hubadilika kuendana na wakati husika.
Hayo yameelezwa bungeni
jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa.
Mbunge huyo aliitaka Serikali kuanzisha Benki ya
waliopekuliwa kwa ajili ya uteuzi ili
kurahisisha zoezi la uteuzi wa
Bodi za Taasisi
na kuziwezesha Taasisi hizo
kwenda na kasi ya Rais kwa
kile alichosema kuwa upekuzi umekuwa kisingizio cha kuchelewesha
uteuzi.
“Upekuzi kwa ajili ya kujaza nafasi
mbalimbali hufanyika kwa wakati husika kutokana na ukweli kwamba utendaji na
mienendo ya maafisa pia hubadilika kutoka wakati mmoja hadi mwingine,” alifafanua Nchemba.
Aidha, alieleza kuwa Wizara
ya Fedha na Mipango ina jumla ya Taasisi 28 ambazo inazisimamia, kati ya hizo, Taasisi Tisa (9) Bodi zake
zimemaliza muda wake.
Nchemba alisema kuwa mapendekezo ya majina kwa ajili ya kujaza
nafasi za Wenyeviti na Wajumbe wa Bodi hizo yamewasilishwa kwenye Mamlaka za
Upekuzi.
No comments:
Post a Comment