HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 05, 2021

Ubalozi wa Saudia Arabia umetoa tani 50 za tende kwa serikali ya Tanzania

 

Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar Zuber akipokea tende kutoka kwa  Kaimu Balozi wa Saudia Arabia nchini Abdulazizi Alasim.

 

Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam

UBALOZI wa Saudi Arabia nchini  umetoa tani 50 za tende ikiwa ni msaada wa kuendeleza mahusiano kati ya nchi hiyo na Tanzania.

Haya yalisemwa jijini Dar es Salaam jana na Kaimu Balozi wa Saudi Arabia nchini Abdulazizi  Alasim wakati akikabidhi msaada huo kwa Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar Zuber.

Alasim alisema  msaada huo wameutoa kwa misingi ya kuendeleza mahusiano baina ya nchi hizo mbili  Saudi Arabia na Tanzania  na kwamba kila mwaka hutoa zawadi.

"Siku hii ni muhimu sana ambayo ubalozi kwa niaba ya serikali ya Saudi Arabia imetoa zawadi ya tende na ni kawaida  ambapo kila mwaka hutoa," alisema Kaimu Alasim.

Aidha Kaimu huyo alimtakia afya njema Mufti Zuber ili aendelee kuwaongoza waumini wa Kiislamu vyema.

Akipokea msaada huo Mufti Zuber aliushukuburu ubalozi wa Saudia Arabia nchini kwa msaada huo na kwamba kila mwaka hupokea tende hizo .

Mufti Zuber alisema tende hizo tani 50  zitatolewa kwa watu mbalimbali na  mwaka huu zimechelewa kutokana na matatizo y virusi vya Covid 19 kuathiri dunia.

" Leo ni siku ya pekee ni nzuri ya kupokea zawadi ya tende tuna ushukuru ubalozi wa Saudia Arabia kwa msaada huu," alisema Mufti Zuber.

No comments:

Post a Comment

Pages