Katibu Baraza la Ulamaa Bakwata Taifa, Sheikh Hassan Chizenga.
Na Upendo Kombe, Dar es Salaam
Licha ya kuzinduliwa kwa chanjo ya uviko 19 Julai 28 2021 ikiwa ni jitihada za kupambana na wimbi jipya la tatu la virusi vya corona, Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA), limesisitiza umuhimu wa kumuomba Mungu ili hatupilie mbali janga hili.
Akitoa tamko la Baraza la Ulamaa Bakwata Taifa mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu Baraza hilo, Sheikh Hassan Chizenga, amesema kuwa waumini wanatakiwa kuzingatia kuhusu chanjo ya uviko 19 kuwa ibada ni jambo la muhimu na lakuzingatiwa hivyo ni vyema ibada zote husika kuendelea lakini kwa kuchukua tahadhari zilizotolewa na wizara ya afya.
Sheikh Chizenga alisema kuwa waumini wanapaswa kungapamoja na matumizi ya vitakasa mikono na vikalio, maji tiririka na sabuni ,kuvaa barakoa ,kukaa umbali wa mita moja kati ya mtu na mtu wakati wa ibada na vikao mbalimbali ili kuzuia madhara ya wahumini kuambukizana ugonjwa huo kabla na baada ya ibada.
Jina chizenga amesema jambo la kuabudu ni la muhimu sababu ndio kiunganishi cha mwanadamu na Mungu hapa ulimwenguni pia amezungumzia uwepo wa chanjo ni fursa kwa waislam kuweza kusafiri kwenda Hijja ikiwa ni utaratibu uliopo kila mwaka.
Amesisitiza kuwa watu ambao wamethibitika kuugua maradhi kama kisukari,pumu,presha na kansa kutokuhudhuria ibada na mikusanyiko mbalimbali ili kujiepusha na maambukizi yanayoweza kutokea badala yake kufanyia swala na dua zao majumbani na haitokuwa vibaya kufanya hivyo maana swawabu za mtu huyo ziko pale pale pia kutokana na ufinyu wa nyumba za ibada baraza[U1] linaomba ruksa ya kutumia barabara na sehemu za wazi kufanyia ibada hizo hata barabarani karibia na misikiti husika.
Amesema ‘’ maandiko yanasema kuwa hakuna sababu ya mtu yeyote kujidhuru au kuwadhuru wengine kukwepa mikusanyiko kama wataalamu wa afya wanavyoeleza ili kulinda afya zetu pia Tanzania ni nchi ambayo Mungu amekuwa akiiepusha na majanga mbalimbali kama kipunga na mengineyo hivyo tuendelee kumuomba Mungu maana ndio silaha yetu’’ Alisema.
Aliongeza kwakuipongeza serikali ya awamu ya sita kupitia rais Samia suluhu Kwakupokea na kuzindua chanjo ya johnson johnson ambayo niya hiyari kwa yeyote mwenye uhitaji kufika kuchanja katika vituo vya afya vyote nchini.
No comments:
Post a Comment