HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 30, 2021

MO AKABIDHI HUNDI YA BIL. 20 KLABU YA SIMBA

 

Mewekezaji na Mwenyrkiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya  Simba, Mohamed Dewji 'MO', akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhi bilioni 20 ya hisa asilimia 49.


Mwekezaji na Mwenyekiti  wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya  Simba Mohamed Dewji " MO", akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Bil. 20 kwa ya hisa asilimia 49 kwa mdhamini wa klabu pamoja na Mwenyekiti wa Klabu, Murtaza Mangungu.

 


Na Upendo Kombe

 

MWEKEZAJI na Mwenyekiti  wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya  Simba Mohamed Dewji leo amekabidhi bilioni 20 kwa ajili ya manunuzi ya hisa asilimia 49 ndani ya klabu hiyo. 

 

Mo amekabidhi bilioni 20 mbele ya mdhamini wa klabu hiyo na kusema kwa miaka minne ametumia bilioni 21.3 na bilioni 5 .3 kila mwaka kwa ajili ya mishahara, usajili wa makocha na wachezaji usafiri, bonus na maandalizi ya timu kabla ya msimu wa ligi kuanza.

"Leo natoa Sh. bilioni 20 rasmi  maana watu walikuwa wakisema mbona Mo haweki hizo fedha, naipenda Simba kwa dhati tangu zamani miaka 20 ijayo itazidi kuimarika bajeti itafikia mara tatu," amesema Mo.


Akizungumza na waandishi wa habari jijni Dar es Salaam Mo alisema "Naipongeza Simba, wanachama na mashabiki wote wenye kuipenda Simba kwa mafanikio ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara nne mfulizo na kufikia hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mara mbili ndani ya miaka mitatu, Simba Queens nayo imeshinda ubingwa wa Ligi ya Wanawake mara mbili mfululizo.’’ Alisema.

 

Mwekezaji huyo alisema kuwa mchakato wa mabadiliko ndani ya klabu hiyo umefikia hatua nzuri "Tumekamilisha mchakato wa mabadiliko, tumepata hati kutoka FCC ya kuturuhusu kumalizia mchakato."

No comments:

Post a Comment

Pages