Na Lydia Lugakila, Ngara Kagera
Mbunge wa Ngara Ndaisaba Ruhoro amefanya ziara wilayani Ngara na kukutana na wadau mbali mbali wakiwemo wa Kijiwe cha Kahawa kwenye Mji wa Kabanga pamoja na kuzungumza na wananchi zaidi ya 50 ambao walipata wasaa wa kupata mrejesho wa utekelezaji wa ahadi zake Wakati wa Kampeni za Uchaguzi mkuu ambapo kiu ya wengi ilikuwa ni kupata huduma ya mita za umeme kutokana na kufuata huduma hiyo Bukoba badala ya kuzipata wilayani humo.
Wananchi hao waliopata nafasi ya kuuliza maswali ya aina mbali mbali baadhi yalipata majibu na mengine yalichukuliwa kwa ajili ya utekelezaji.
Aidha baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wananchi hao ni pamoja na kutaka kujua ni sababu zipi zinazofanya Mita za umeme kutouzwa wilayani Ngara na baadala yake zinauzwa Bukoba hali inayoleta usumbufu kwa wananchi wanaohitaji mita hizo.
Miongoni mwa wauliza maswali ni pamoja na mzee Said Manywele, huku mbunge wa jimbo hilo Ndaisaba Ruhoro akiahidi kumaliza changamoto hiyo.
Baada ya hatua hiyo mbunge huyo, amefanya mawasiliano na Kaimu mkurugenzi mkuu wa TANESCO na baada ya mawasiliano hayo, TANESCO imeahidi kutoa maelekezo mkoani ili mita zifikishwe Ngara haraka ili wananchi waanze kupata huduma kutokea Ngara.
RUHORO ameishukuru TANESCO kwa utendaji wa kazi mzuri uliotukuka na kwa kuwa Tayari kujibu kero mbali mbali za wananchi ikiwa ni pamoja na kuzifanyia kazi.
No comments:
Post a Comment