Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amewaondoa hofu na kuwahakikishia
Watanzania Chanjo ya Ugonjwa Covid-19 ni salama huku akibainisha
kuipokea kwa hiari ili kujikinga na wimbi la tatu la ugonjwa huo.
Ameyasema
hayo jijini humo katika kikao kazi kilichomkutanisha na watendaji wa
afya wa Jiji hilo, Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi wa manispaa zote,
Makatibu tawala na watendaji wengine wa lishe kilichojadili mikakati ya
kujikinga na ugonjwa huo pamoja na lishe kwa Jamii.
Amesema
wananchi wa Dar es Salaam na watanzania wanatakiwa kuondoa hofu kuhusu
chanjo hiyo kwani tangu wako wadogo hakuna chanjo waliyochanjwa
iliyotengenezwa nchini hivyo wanatakiwa kuipokea kwa hiari kuchanjwa
lengo likiwa kukabiliana na janga hilo.
"
Niwatoe hofu Watanzania tumepatiwa tuipokee kwa hiari katika chanjo
zote tulizopewa hajitengenezwa hapa ondoeni hofu chanjo hii iko salama
tuchanje kwa hiari tujikinge na Corona binafsi najisikia vizuri baada
ya kuchanjwa," amesema Makalla.
Amempongeza
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy
Gwajima kwa kuendelea kukabiliana na ugonjwa kwa kutoa miongozo
mbalimbali ya kujikinga pamoja na kutoa maelekezo kwa watendaji wa
Serikali na mamlaka husika kuchukua hatua.
RC
Makalla amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa umauzi wake wa kukubali
kuingizwa chanjo nchini kwa ajili ya kujikinga na Corona pamoja na
kuonyesha mfano wa kuchanjwa chanjo ya ugonjwa huo kwa hiari huku
akisisitiza kufanya hivyo ni kukubaliana na ukweli wa dunia kuhusu
ugonjwa huo.
Ameiagiza kamati ya ulinzi na
usalama za mkoa kusimamia kanuni na miongozo ya kujikinga na ugonjwa huo
ikiwemo daladala kutosimamisha abiria na watakopanda kuvaa barakoa
pamoja na Kivuko cha Kigamboni kuzingatia kanuni hizo.
RC
Makalla amewaagiza wakuu wa wilaya kuendelea kusimamia kanuni, shera na
miongozo ya kupambana na Covid 19 pamoja na kutenga fedha za kutoa
elimu na mafunzo kwa maafisa lishe ili kuwaongezea ujuzi katika shughuli
zao.
Kwa upande wake Waziri Gwajima
ameupongeza mkoa huo kwa hatua mbalimbali unaozichukua katika
kukabiliana na ugonjwa huo na kusisitiza chanjo hizo zisichukue siku 10
kuwafikia wananchi na kwamba maeneo yatakayolegalega kuzitoa
watazichukua.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni
kwa niaba ya wakuu wa wilaya waliopo Dar es Salaam ametoa shukrani kwa
mkoa kwa kuandaa kikao hicho chenye lengo la kujikinga na ugonjwa huo
nchini.
No comments:
Post a Comment