HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 01, 2021

KIPANGA AJIVUNIA MAFANIKIO SEKTA YA ELIMU

  Katibu Mtendaji wa Vyuo Vikuu Tanzania Prof. Charles Kihampa,akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kufunga  Maonesho ya 16 ya Sayansi na Teknolojia katika viwanja vya Manzi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Makamu Mwenyekiti Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Mgone, akitoa hotuba yake wakati wa kufunga Maonesho ya 16 ya Sayansi na Teknolojia katika viwanja vya Manzi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga (kushoto) akipata maelezo alipotembea banda la Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU). 

 Baadhi ya wanafunzi wakipitia taarifa mbalimbali kuhusu elimu ya juu walipotembelea maonesho ya Vyuo Vikuu Tanzania.
 Baadhi ya wanafunzi wakifanya udahili katika viwanja vya Mnazi Mmoja katika Maonesho ya Vyuo Vikuu.
Wanafunzi wakifanya udahili katika banda la Chuo kikuu Mzumbe.
Wakuu wa taasisi wakiwa katika hafla ya kufunga
Maonesho ya 16 ya Sayansi na Teknolojia katika viwanja vya Manzi Mmoja jijini Dar es Salaam.

 

 

 Na Upendo Kombe, Dar es Salaam

  
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga, amesema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita sekta ya elimu nchini imepata mafanikio makubwa kutokana na ongezeko la wanafunzi wanaodahiliwa vyuo vikuu.

Akizungumza wakati wa kufunga Maonesho ya Vyuo Vikuu Tanzania yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam amesema miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na kuongezeka kwa wanafunzi wanaodahiliwa katika shahada ya kwanza kwenye vyuo vya elimu ya juu kutoka 66,000, 64,000 mwaka 2015/16 hadi 87,934 mwaka 2021.


Kipanga  amesema idadi ya wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu imeongezeka kutoka wanafunzi 125,126 mwaka 2015 hadi 149,506 2020.

Aidha amesema katika kipindi hicho miundombinu ya kufundishia na kujifunzia imeboreshwa katika ngazi zote za elimu ikiwemo ujenzi pamoja ukarabati wa madarasa, kumbi za mihadhara, maabara, maktaba, hosteli na ununuzi wa vifaa vya utafiti pamoja na vifaa vya kufundishia na kujifunzia. 

 

“tumeendelea kuimarisha mifumo ya udhibiti ubora ili kuhakikisha vyuo vikuu vinatoa elimu bora ya kiushindani ndani na nje ya nchi" Amesema Kipanga.   

     

Naye Katibu Mtendaji wa Vyuo Vikuu Tanzania Prof. Charles Kihampa, amewashukuru wadau waliofanikisha Maonesho ya 16 ya Elimu ya juu Sayansi na Teknolojia ambayo kauli mbiu  ya mwaka huu ni kuendeleza kukuza na kudumisha uchumi wa kati kupitia elimu ya juu sayansi na teknolojia.

 

Kihampa amesema  lengo la maonesho haya ni  kutoa fursa kwa taasisi zinazoshiriki ili kujitangaza na kuonesha huduma mbalimbali zinazofanya pamoja mchango wao katika kuendeleza jitihada za Serikali ili kukuza na kudumisha uchumi wa kati kupitia elimu ya juu.

 

“Mgeni rasmi umejionea baadhi ya mabanda machache ambayo umeweza kuyapitia na kuona jinsi ambavyo taasisi zetu zimekuwa zikifanya kazi, lengo la maonesho hayo ni  kutoa fursa kwa taasisi hizi ili kujitangaza kuonesha huduma na kazi mbalimbali wanazofanya" Amesema Kihampa.

 

Pia Kihampa amesema "Kupitia maonesha haya wananchi na wadau mbalimbali wa elimu ya juu wamepata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zinazofanya na taasisi za elimu ya juu na hivyo kuweza kufanya majadiliano na makubaliano ya namna ya kupata huduma za kiushauri katika biashara, usanifu wa majengo, ujenzi, uhandisi, kilimo, afya na kwa wale wanaotegemea kujiunga na elimu ya juu kufanya maamuzi na uchaguzi sahihi wakati wa kuomba udahili, kuanzia wale wanaotaka kusoma ngazi ya cheti, diploma, shahada ya kwanza mpaka shahada ya juu kabisa (PHD). 

 

Katika maonesho hayo kwa upande wa shahada ya kwanza waombaji 52,336 wametuma maombi yao ya udahili katika vyuo mbalimbali kwa awamu hii ya kwanza katika siku sita za maonesdha hayo.


Prof. Kihampa aliongeza kuwa katika maonesho hayo  taasisi 74 zimeshiriki ikilinganisha na 67 zilizoshiriki mwaka jana. 

No comments:

Post a Comment

Pages