HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 06, 2021

Watanzania waaswa kutumia chai asili

Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam

Mkurungezi wa Taasisi inayojishughulisha na utoaji wa tiba  asili Cornewell Tanzania Elizabeth Lema, amesema unywaji wa chai ya asili iliyotegenezwa kwa kiwango kinachotakiwa inamuwezesha watumiaji kuimarisha kinga za mwili yao.

Pia amewashauri Watanzania kutumia chai ya asili inayotegenezwa na mimea ya asili kwa lengo la kuuweza mwili kupata Kinga sahihi na yenye virutubisho.

Haya amesema  katika maonyesho ya 45 ya Kimatafa ya Biashara DTIF yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Jijini Dar es salaam,

Amesema zipo  aina nyingi  za chai ya asili zikiwamo za  Digestive tea, Diabetes tea,Mango leaves tea,Giele Herbal tea, Eucalyptus Herbal tea na Cemon Leaves tea.

Mkurugenzi hiyo aliipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuthamini mchango wa tiba za asili na kwamba  wataendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha wanafanya kazi kwa usahihi ili kuimarisha afya za jamii iliyowazunguka.

 Amesema kuna bidhaa nyingine ambazo zinatumia mimea ya asili kutibu magonjwa mbalimbali ambazo zimeboreshwa ili kukuwezesha mtumiaji kupata yenye usahih.

"Kuna magonjwa mengi ambayo yanaweza kutubika kupitia miti dawa za asili na Watanzania wakaendelea na shuguhuli zao za kujiingizia kipato wao na Taifa kwa ujumla," ameseme Mkurugenzi huyo.

Amewataka  Watanzania kutembelea bada lao lililopo katika maonyesho hayo ili waweze kupata maelezo sahihi kutoka kwa wataalamu huku akiipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kutambua mchango wa tiba asili inayotokana na mimea.

No comments:

Post a Comment

Pages