Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar, Omar Said Shaaban akikagua karafuu kisiwani Pemba.
Na Mwandishi Wetu, Pemba
WAZIRI
wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar,
Omar Said Shaaban jana Julai 12, 2021 amefanya ziara kwenye vituo
vitatu vya ununuzi wa karafuu kisiwani Pemba.
Vituo hivyo vya ununuzi vipo wilayani, Chake Chake na Wete kisiwani Pemba.
Akizungumzia
ziara hiyo, Waziri Shaaban amesema lengo ni kujionea hali ilivyo kwenye
vituo pamoja na kuwasikiliza wakulima na watendaji changamoto
wanazokabiliana nazo.
"Nimetoa
ufafanuzi wa baadhi ya changamoto hizo na maelekezo kwa yale ambayo
nimeyaona yana upungufu upande wetu wa serikali na watoa huduma
tunaoshirikiana nao kwenye vituo.
"Nimeahidi
kuzitatua changamoto nyengine ambazo zinahitaji kujadiliana na wenzetu
wengine lakini lengo ni lile lile kuhakikisha mchakato wa manunuzi
unaendelea kwa ufanisi bila ya vikwazo katika msimu huu wa karafuu"
amesema wazri huyo.
No comments:
Post a Comment