Mbunge mteule wa jimbo la Konde-Pemba, Sheha Mpemba Faki.
Chama cha ACT Wazalendo kimeona taarifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia mitandao ya kijamii kuhusu kujiuzulu kwa Mbunge mteule wa CCM, Sheha Mpemba Faki wa Jimbo la Konde-Pemba. Chama kinafuatilia kwa karibu kuhusu taarifa hii, ikiwemo kusubiri kupokea taarifa rasmi toka Tume ya Uchaguzi (NEC).
Hivyo, Chama kinaomba na kuwasihi wanachama wake, wapenzi na wananchi kwa ujumla wawe watulivu kupisha na kutoa nafasi kwa viongozi wa Chama Taifa kukamilisha suala hili katika njia ya utulivu na ya mazungumzo ikihusisha wadau wote muhimu.
Chama kitatoa taarifa kamili ya msimamo wake kuhusu suala hili baada ya kikao cha dharura cha Kamati Kuu kinachotegemewa kuketi wakati wowote mwishoni wa wiki hii.
Chama kinatanguliza shukrani kwa ushirikiano.
No comments:
Post a Comment