HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 03, 2021

MBUNGE JIMBO LA NKENGE WILAYANI MISENYI MKOANI KAGERA AMEMPONGEZA RAIS SAMIA UTEUZI WA WAKURUGENZI WATENDAJI NCHINI

 

Aliyekuwa mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Misenyi mkoani Kagera, Innocent Mkandala, akizungumza na wananchi pamoja na watumishi wa halmashauri hiyo na kuwapongeza kwa ushirikiano.

 

Na Lydia Lugakila, Misenyi

Mbunge wa jimbo la Nkenge wilayani Misenyi mkoani Kagera Florent Kyombo amempongeza Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa uteuzi alioufanya kwa wakurugenzi watendaji wa halmashauri nchini, huku akitaja halmashauri ya Misenyi kunufaika na aliyekuwa mkurugenzi wa wilaya hiyo Innocent Mkandala aliyehamishiwa wilayani Biharamulo Mkoani humo kwa  uongozi wake uliotukuka.

Mh, Florent Kyombo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi wa kata za Kyaka Mushasha na Bulembo wilayani waliojitokeza kusafisha eneo la ujenzi wa hospitali mpya ya wilaya ya Misenyi.

"Tunashukuru Rais Samia kwa kufanya mabdiliko ya wakurugenzi na wengi wamebaki nje lakini mkurugenzi wetu amebaki ndani ya kazi, Innocent Mkandala amepelekwa wilaya ya Biharamulo kwa hiyo tunasema asante mama yetu kwa imani na mkurugenzi hatuwezi badilisha ila tutamkumbuka kwa utendaji wake ulio mzuri" alisema mbunge Kyombo.

Mbunge huyo ameeleza kuwa   mkurugenzi huyo atakumbukwa pia kwa usimamizi mzuri wa mapato na mtumizi katika wilaya hiyo pamoja na usimamizi mzuri kwa wenzake waliomsaidia huku akimuomba mkurugenzi huyo kumfunda  anayechukua mikoba yake ili waweze kufanya naye kazi vizuri kama ambavyo yeye alikuwa na uchungu wa maendeleo kwa wilaya hiyo.

Aidha aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo Innocent Mbandwa Mkandala amehamishiwa wilaya ya Biharamulo na mikoba yake kuchukuliwa na waziri Khachi   Kombo.

Kwa upande wao baadhi  watumishi wa halmashauri hiyo  akiwemo  Julian Joseph Tarimo mkuu wa idara ya mipango takwimu na ufuatiliaji amesema tangu ahamie katika halmashauri ya wilaya ya Misenyi mwaka  2020 mwezi Desemba amebahatika kufanya kazi na Mkurugenzi Mtendaji huyo kwa kipindi cha miezi 7 na kujionea utendaji wake ulivyo wa tofauti.

 "Mukandala ni tofauti kabisa na wakurugenzi wote niliowahi kufanya nao kazi kwanza ni  mkurugenzi mchapa kazi mwadilifu  mwenye hofu ya Mungu na anayejali maslahi ya wananchi haki za watumiaji pia ni mtu aliyependa kufahamu idara zake zinavyofanya kazi na mfuatiliaji wa miradi ya maendeleo na asiyetaka ubabaishaji zaidi ni mtu aliyekuwa  kunyoosha mambo na asiyependa ubabaishaji, binafsi namtakia kila la kheri kwenye kituo chake kipya akaendeleze yale mazuri aliyoyafanya wilayani Missenyi" alisema Tarimo.

Hata hivyo kwa upande wake mkurugenzi huyo Innocent Mkandala amewashukuru watumishi wa halmashauri hiyo pamoja na wananchi kwa ushirikiano waliouonyesha kwa kipindi chote.

Ikumbukwe kuwa Agosti 2, 2021 Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wakurugenzi watendaji wa halmashauri za jiji, Manispaa, na wilaya.

No comments:

Post a Comment

Pages