Msanii
na Video Vixen Masha Love akiwa ameshikana mkono na Mkurugenzi wa
Sabuni ya Saffron baada ya kusaini mkataba wa miezi sita wenye thamani
ya Sh milioni 40 wa kuwa balozi wa bidhaa hiyo.\
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Msanii
na Video Vixen Masha Love amesaini mkataba wa miezi sita wenye thamani
ya Sh milioni ya 40 wa kuwa Balozi wa Sabuni ya Saffron.
Akizingumza
na wanahabari leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya utiaji saini
mkataba huo msanii huyo amesema anawashukuru wahusika wa sabuni hiyo kwa
kumpatia ubalozi huo na kwamba atautumia katika kuwakwamua wanawake
wasio na ajira katika maeneo atakayotembelea kutangaza bidhaa hiyo.
"
Nawashukuru Saffron kwa kunipa mkataba kutangaza bidhaa zao watu
wamekuwa wakinichukulia tofauti kwenye mitandao wananiona chizi kumbe
timamu ubalozi nitautumia kuwakomboa wenzangu niliyokuwa nao wapate
ajira," amesema Masha Love.
Amebainisha kuwa
katika mikoa atakayopita kuitangaza sabuni hiyo wanawake watapata fursa
ya kupata uwakala wa bidhaa hivyo amewashauri kujitokeza kwa wingi na
kwamba analishukuru Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa kumfanya kuwa
na maadili na heshima.
Ameongeza kuwa katika
maisha yake amepitia changamoto nyingi na kwamba ubalozi alioupta
atautumia kuwarekebisha wenzio ambao hawajatoka katika maisha aliyokuwa
akiishi kabla hajajulikana.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Sabuni hiyo, Ester Dalali amesema wameamua kumpatia
ubalozi huo msanii kwa kuwa ni mtu mwenye kujiamini na kuthubutu kufanya
jambo hivyo anaamini atasaidia kuitangaza vyema bidhaa hiyo kwa jamii.
Mkurugenzi
huyo amefafanua kuwa katika muda wa mkataba huo msanii Masha Love
atapata fursa ya kuishi kwenye nyumba yenye thamani ya Sh Milioni 97
huku akiwashauri watu kuchangamkia fursa ya kuwa mawakala wa sabuni
hiyo.
No comments:
Post a Comment