Mtaalam wa Maabara kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama Kanda ya Mashariki, Fimbo Emmanuel, akimtoa damu, Murtadha Rashid mmoja wa waumini wa Juimuiya ya Khoja Shia Ithnasheri Jamaat (KSIJ), wakati wa kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha kiongozi wa dhehebu hilo Imamu Hussein, kwenye msikiti wa KSIJ jijini Dar es Salaam. (Na Mpiga Picha Wetu).
Mtaalam wa Maabara kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama Kanda ya
Mashariki, Gisbert Ruseneka, akimtoa damu, mmoja wa waumini wa Juimuiya
ya Khoja Shia Ithnasheri Jamaat (KSIJ), wakati wa kuadhimisha kumbukumbu
ya kifo cha kiongozi wa dhehebu hilo Imamu Hussein, kwenye msikiti wa
KSIJ jijini Dar es Salaam. (Na Mpiga Picha Wetu).
Mtaalamu wa Maabara ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Samuel Mluma,
akiishukuru KSIJ na Taasisi ya Ebrahim Haji kwa kuthamini na kuijali
jamii ya wenye uhitaji na kujitolea kuchangia damu, ambayo mahitaji yake
ni makubwa.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uchangiaji damu, iliyofanyika Msikiti wa KSIJ katikati ya jiji.
NA MWANDISHI WETU
WANACHAMA
wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-Asheri Jamaat (KSIJ) kwa kushirikiana na
Taasisi ya Ebrahim Haji, wamejitolea kuchangia damu kwa Mpango wa Taifa
wa Damu Salama, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo
cha Imamu Hussein.
Meya
wa Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto, alihudhuria hafla hiyo ya
uchangiaji damu, iliyofanyika Msikiti wa KSIJ katikati ya jiji, ambako
aliwapongeza Wana Jumuiya hao kwa kudumisha utamaduni chanya wa
kusaidia wenye uhitaji ikiwemo uchangiaji damu huo.
Meya
Kumbilamoto alibainisha kuwa, KSIJ na Ebrahim Haji, wameionesha jamii
ya Watanzania namna wanavyopaswa kujitoa kwa ustawi wa maisha wenye
uhitaji, na kwamba damu iliyochangwa na Wana Jumuiya hao, inaenda kuokoa
maisha Wengi miongoni mwa wahanga wa ajali, wamama wajawazito na
wagonjwa wa kansa ya damu.
Kumbilamoto
aliwapongeza KSIJ na Ibrahim Hajj na kuzitaka taasisi zingine na jamii
kuiga utamaduni chanya unaofanywa na wanachama hao, ambao unalenga sio
tu kuakisi yalivyokuwa maisha ya kiongozi wao Imamu Hussein, bali kuunga
mkono jitihada za Serikali katika kutatua changamoto mbalimbali
zinazowakabili watu wake.
"Nitoe
wito kwa jamii, kuiga mfano wa KSIJ na Ebrahim Haji, ambao wamekuwa
wakijitolea damu kila mwaka. Awali walikuwa wakitoa mara moja kwa mwaka
kila wanapokuwa na maadhimisho haya, lakini Sasa wamekuwa wakichangia
damu kila wanapoombwa kufanya hivi.
"KSIJ
na Ebrahim Haji, wameenda mbali zaidi kwa Sasa kwa kujitosa katika
utatuzi wa changamoto mbalimbali, hasa zinazoikabili sekta ya Elimu na
Afya nchini, walikotoa vifaa tiba, vifaa vya elimu na hata ujenzi na
maboresho ya miundombinu kwenye Sekta hizo muhimu kwa maendeleo ya
jamii," alisisitiza Meya Kumbilamoto.
Akizungumza
kwa niaba ya KSIJ, Ain Sharrif, ambaye ni Mwanachama Mwandamizi Jumuiya
hiyo, alisema utamuduni huo wa kuchangia damu wamekuwa wakiufanya kila
(Mwezi Muharram) wanapoadhimisha kifo cha kiongozi wao Sayyidina Hussein
(Imamu Hussein), aliyekufa kwa kujitoa mhanga yapata miaka 1400 iliyopita.
"Tumekuwa
tukifanya hivi tangu mwaka 2008, lengo likiwa ni kuyaishi maisha ya
Imamu Hussein, ambaye alisimama imara katika kujitolea kwa ustawi wa
maisha ya aliowaongoza na jamii iliyomzunguka. Nasi tunafanya haya na
mengineyo ili kufuata nyayo zake na kutii wosia zake.
"Leo
tunavyo vituo vitatu vinavyochangia damu jijini Dar es Salaam, ambapo
pia kupitia Hospitali ya Ibrahim Hajj tumekuwa tukisaidia mamia ya
watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kwa kuwapatia misaada
mbalimbali kulingana na mahitaji yao, sambamba na huduma za matibabu,"
alisema Sharrif.
Naye
Mtaalamu wa Maabara ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Samuel Mluma,
aliishukuru KSIJ na Taasisi ya Ebrahim Haji kwa kuthamini na kuijali
jamii ya wenye uhitaji na kujitolea kuchangia damu, ambayo mahitaji yake
ni makubwa.
"Kila mwaka
KSIJ na Ibrahim Hajj wamekuwa wakichangia zaidi ya Unit 400 za damu
kupitia maombolezo yao haya ama tunapowahitaji.
"Mahitaji nchini ni
makubwa, takribani chupa 250,000 kwa mwaka, kwahiyo tunapowapata watu na
Taasisi za mfano wa Kama KSIJ na Ibrahim Hajj, tunakuwa na uhakika wa
makusanyo ya kutosha kukidhi mahitaji," alisema Mluma.
No comments:
Post a Comment