HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 29, 2021

Simba SC yazindua Simba SC App

Na Hussein Ndubikile,  Dar es Salaam

Klabu ya Soka ya Simba imezindua  App  yake (yenye lengo la kuwawezesha mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kupata  taarifa mbalambali zinazohusu timu hiyo.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam katika Hafla ya uzinduzi huo Msemaji wa klabu hiyo Ezekiel Kamwaga amesema Simba App ni jukwaa la  kidijitali litakalokuwa linatoa taarifa za timu hiyo kwa usahihi, haraka na kwa wakati hivyo Wanasimba watapata tarifa za usajili, ratiba za mechi za ndani na nje ya nchi.

Simba SC hatuaki kubaki nyuma leo tunazindua hii App kidijitali mashabiti wetu watapata taarifa za mechi, usajili na jezi App hii itasaidia kuingizia timu mapato," amesema Kamwaga.

Ameabinisha kuwa kupitia App hiyo mashabiki wote watafikiwa hata wanaotumia simu za tochi watapata taarifa endapo watalipa Sh 2000 kwa ajili ya kujisajili hivyo itataleta chachu ya kuongeza mapato ya timu.

Amesisitiza kuwa wameamua kuzindua App hiyo kuendana na mapinduzi ya kidijitali na kwamba Simba inakuwa klabu ya kwanza Tanzania kwenda na mifumo ya kidijitali hivyo taarifa za Simba Day zitatangazwa kwenye App yao pamoja za taarifa za mechi wanayocheza leo na klabu ya daraja la kwanza nchini Morocco.

Kwa upande wake Mtaalam aliyetengeneza Simba App ambaye pia ni Mtaalam wa Ubunifu wa Teknolojia kutoka Myelimu, Given Edward amesema uzinduzi huo umefanyika kwa kuzingatia ukubwa wa klabu hiyo kwani sio mashabiki wote wanaoingia uwanjani hivyo hata walio nje watapata taarifa za klabu.

Amefafanua kuwa mshabiki au mwanachma anatakiwa kujisajili kabla hajaingia katika App hiiyo kwa kulipia kiasi hicho cha fedha kwa mwezi au kufanya malipo ya mwaka mzima kwani atapata maelekezo katika hatua atakayopitia akiyatimiza ndipo ataanza kupatiwa taarifa za klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages