Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam
HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (NMH), imesema kuwa juzi ilipokea majeruhi watano na mwili mmoja wa marehemu kati ya mareruhi hao wanne ni Askari wa Jeshi la Polisi na mlinzi wa kampuni binafisi ya SGA katika tukio liliotokea katika majibizano ya risasi.
Tukio hilo lilitokea katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam karibu na Ubalozi wa Ufaransa.
Katika taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma wa Muhimbili Aminiel Aligaesha ilisema juzi kuanzia majira ya saa saba mchana walipokea maharuhi hao wakiwa na majeraha makubwa na wengine madogo sehemu mbalimbali za miili yao.
Amesema mara baada ya kupokelewa, askari wawili wenye umri wa miaka 41 na miaka 49 walikua na majeraha makubwa katika sehemu mbalimbali za mwili pamoja na viungo vya ndani ambapo walfanyiwa upasuaji wa haraka ambao ulienda vizuri.
"Askari wa tatu ( 35) naye alipata majeraha mbalimbali makubwa na madogo katika maeneo ya mikono na mgongoni ambaye alipewa huduma stahiki na kufungwa vidonda," amesema Mkuu huyo wa Kitengo.
Ameongeza kuwa askari wa nne (46), alitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani kwakua alikua na majeraha madogo.
Aligaesha amesema mlinzi wa SGA (42) naye alikuwa na majeraha ambayo hayakuhitaji upasuaji hata hivyo alilazwa wodini na kwamba aliruhusiwa jana ambapo ataendelea na matibabu akiwa nyumbani.
Mkuu huyo wa Kitengo ameeleza kuwa wamebakiwa na majeruhi watatu ambao wanaendelea kupata matibabu na hali zao zinaendelea kuimarika.
Amesema mwili wa marehemu walioupokea kutoka katika tukio tukio hilo ni Mlinzi wa SGA na umehifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti.
No comments:
Post a Comment