DAR ES SALAAM, TANZANIA
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa, leo Agosti 27, ametembelea mazoezi ya timu ya Kamati ya Amani (viongozi wa dini), yaliyofanyika Viwanja vya Jakaya Kikwete Youth Park, Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.
Timu hiyo itacheza mechi maalum dhidi ya Wachambuzi wa Michezo siku ya Jumatano, Septemba Mosi,k Uwanja wa Azam Complex, Chamazi kuanzia saa 1:00 usiku.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi akisindikizwa na Waziri wa Afya, Dorothy Gwajima.
Mwamuzi wa mechi atakuwa Afande Mstaafu Suleiman Kova, marefa wasaidizi ni Mzee Azim Dewji na Afande Jumanne Mulilo, ambaye ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Sheikh Abubakar Zubeiry, anatarajia kuwa mwamuzi wa akiba wa pambano, linalolenga kuhamasisha uungaji mkono chanjo ya UVIKO-19, inayotolewa kwa hiari kwa makundi yote ya kijamii nchini.
Waziri Bashungwa aliambatana na Mkurugenzi wa Michezo, Yusuph Singo na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidao.
No comments:
Post a Comment