Ataka Wamiliki na LATRA kusimamia level seat na abiria wote kuvaa Barakoa
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla (pichani) ametoa tamko la kusisitiza matumizi sahihi ya Barakoa kwa kila abiria wote wanaopanda kwenye vyombo vya usafiri huku akiwataka Wamiliki wa Vyombo hivyo kuwaelekeza madereva na makondakta kuepuka kubeba abiria asiavaa Barakoa.
RC
Makalla ametoa msisitizo huo wakati wa kikao Cha Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Mkoa kilichoketi kupitia tathimini ya utekelezaji wa mwongozo
ukiotolewa na Wizara ya Afya juu ya kujikinga na Corona na kuendelea
kusitiza Suala la level seat.
Makalla amesema kumekuwa na ulegevu wa usimamizi kwenye baadhi ya
maeneo ambapo ametoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi, Wakuu wa Wilaya na
LATRA kuhakikisha wanasimamia ipasavyo mwongozo wa Wizara ya Afya.
Kutokana
na changamoto za usafiri kwa wanafunzi, RC Makalla ameruhusu Daladala
kubeba Wanafunzi watano watakaosimama lakini kwa kigezo Cha wanafunzi
hao kuwa wamevaa Barakoa.
Aidha
RC Makalla ameendelea Kusisitiza Wananchi kuepuka Mikusanyiko isiyokuwa
na lazima na Kama ikitokea Kuna ulazima taratibu zote za kujikinga
zizingatiwe.
Kuhusu suala
la Chanjo RC Makalla amefurahi kuona Wananchi wamekuwa na mapokeo
makubwa ya kupokea chanjo ambapo kwa Mujibu wa Mganga mkuu wa Mkoa huo
adi kufikia Jana tayari Wananchi 10,000 wamefanya booking na wanahofia
Chanjo zitawahi kumalizika.
No comments:
Post a Comment