Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara
(TANROADS), Mkoa wa Mwanza Mhandisi Vedastus Maribe akifungua rasmi
mafunzo ya wakandarasi wanawake wanaotumia teknolojia stahiki ya nguvu
kazi katika utengenezaji wa barabara jijini Mwanza.
Sehemu ya wakandarasi wanawake wanaotumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi katika utengenezaji barabara wakiwa katika mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Mwanza.
Na Mwandishi Wetu
IMEELEZWA
kuwa kampuni nyingi za wakandarasi wanawake wanaotengeneza barabara kwa
kutumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi zitafanikiwa endapo
wakandarasi hao watakuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS)
Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Vedastus Maribe wakati akifungua mafunzo
wakandarasi wa barabara kwa kutumia teknolojia stahiki jijini Mwanza.
Mhandisi
Maribe amewaasa wakandarasi hao kujielimisha vya kutosha kabla ya
kuomba kazi ujenzi na ukarabati wa miradi ili wapate faida na kukuza
kampuni zao.
"Jazeni
vizuri zabuni kwa kuzingatia ukubwa wa kazi, imarisheni usimamizi ili
kazi zikamilike kwa wakati, malengo yatimie na kujikomboa kiuchumi,"
Mhandisi Maribe.
Amehimiza wakandarasi hao kujisajili ili wapewe miradi mingi na hivyo kukua toka wakandarasi wadogo hadi wakubwa.
Naye
Mratibu wa Mafunzo hayo Mhandisi Liberatha Alphonce amewataka
wakandarasi hao kuongeza mtandao wa wadau ili kubadilishana uzoefu,
ujuzi na fursa.
Alisema
Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ina imani na kazi zinazofanywa na wanawake
hivyo itaendelea kuwajengea uwezo na kuwapa miradi mingi kutokana na
bidii zao.
Zaidi ya
wakandarasi wanawake 80, toka mikoa ya Mwanza, Simiyu, Mara, Geita na
Kagera wanashiriki mafunzo hayo ambayo pamoja na mambo mengine
yatawajengea uwezo katika ujazaji wa zabuni, taratibu za kusajili
kampuni, sheria ya manunuzi, namna ya kutumia mfumo wa manunuzi (TANePS)
na usimamizi wa mikataba.
No comments:
Post a Comment