Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu (Uwekezaji) William Tate Ole Nasha, akifungua Kongamano la
Kaizen Barani Afrika kwa mwaka 2021 (AKCA2021) linalofanyika kuanzia
Agost 24 hadi 26.
Hussein Ndubikle, Dar es Salaam
Serikali
imesema kuwa imeanza kuimarisha sera, kanuni, sheria, taratibu na
miongozo ili kujenga sekta binafsi imara na madhubuti huku ikibainisha
kuendelea kufanya mapitio katika sera ya taifa ya kumlinda mlaji, sera
ya taifa ya ubora pamoja na Sheria ya Uwekezaji.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu (Uwekezaji) William Tate Ole Nasha kwa niaba ya Waziri wa
Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo wakati akifungua Kongamano la
Kaizen Barani Afrika kwa mwaka 2021 (AKCA2021) linalofanyika kuanzia
Agost 24 hadi 26 mwaka huu linaloshirikisha mataifa zaidi ya 20
yanayotekeleza falsafa hiyo.
Amesema Serikali
inatambua umuhimu na jukumu lake la kuimarisha sekta hiyo ndio maana
Rais Samia Suluhu Hassan anaendelea kuweka na kuimarisha sera na
miongozo pamoja na mazingira wezeshi ili kuhakikisha viwanda vinafanya
kazi kwa ufanisi hali itakayosaidia kuimarisha sekta binafsi nchini.
"
Lazima tuangalie namna ya kukuza sekta binafsi hasahsa viwanda
vitengeneze ajira na kodi tukiimarisha sekta hii itachangia kiasi
kikubwa katika pato la taifa Serikali kazi yake ni kuweka sera, miongozo
na mazingira wezeshi," amesema Naibu Waziri Ole Nasha.
Amebainisha
kuwa katika kuhakikisha hilo linafanikiwa Serikali ianendelea kuboresha
miundombinu ya viwana na kwamba inafanya majadiliano na wadau ili
kufungua fursa za kibiashara.
Amesisitiza kuwa
kongamano hilo litasadia kuimarisha sekta ya viwanda na biashara na
kuwakukumbusha watendaji wa wizara hiyo na sekta binafsi kutambua namna
gni ya kushughulikia na kusimamia majukumu yo kikamilifu.
Ameongeza kuwa kauli mbiu ya kongamano hilo ni fursa
za kuharakisha maendeleo ya Viwanda na Biashara Barani Afrika na kwamba
limebeba ujumbe unaosisitiza uzingatiwaji wa matumizi ya Falsafa ya
KAIZEN (Uongezaji Ubora & tija - QPI) na Teknolojia za Dijitali,
katika Uanzishaji na Uendelezaji wa Viwanda vidogo na Biashara Ndogo na
shughuli za kiuchumi majumbani ili kukuza uchumi wa ndani Barani Afrika.
Aidha,
amesema Serikali inaamini katika falsafa hiyo na kwamba imejiunga
katika mpango huo ili kufikia malengo iliyojiwekea ikiwemo biashara na
sekta ya viwanda lengo likiwa kuchochea pato la taifa.
Kwa
upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amabaye pia ni
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo amesema falsafa hiyo ya
Kiajapani zinasaidia kuratibu masuala mbalimbali ikiwemo kuongeza
ufanisi na kuwapa fursa viongozi kujifunza namna falsafa zinaweza
kuisaidia jamii.
Mkuu
wa wilaya huyo amesema anatamni falsafa hiyo ifike katika ngazi za
maispaa ili zitumike kuwajengea uwezo wanachi hasa wanaochukua mikopo ya
vikundi kuanzisha biashara na viwanda vidovidogo.
No comments:
Post a Comment