Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba akizindua Tume ya Kufanya
Tathimini Mapitio na Maboresho ya Mifumo ya Ukusanyaji Mapato na
Matumizi ya Serikali.
Profesa Nehemiah Usoro akizungumza katika uzinduzi wa tume hiyo.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amezindua Tume ya Kufanya
Tathimini Mapitio na Maboresho ya Mifumo ya Ukusanyaji Mapato na
Matumizi ya Serikali huku akibainisha uzoefu unaonesha nchi
zilizoendelea zimepata mafanikio sababu ya kufanya mapitio na maboresho
ya mifumo hiyo hivyo ni vyema nchi ikafanya hivyo.
Akizindua
tume hiyo jijini Dar es Salaam Waziri Dk. Nchemba amesema nchi
zilizoendelea zimefanikiwa kuwa na kiwango bora cha ukusanyaji mapato
kutokana na kuwa mifumo thabiti na kwamba anaamini tume hiyo itatekeleza
majukumu yake kikamilifu kwani ina wajumbe wenye uzoefu kwenye masuala
ya fedha, mipango, mapato na matumizi.
"
Tumeamua tupate wajumbe wa tume wa kuangalia mifumo ya mapato na
matumizi watapitia mifumo na kufanya tathmini na maboresho itakayosaidia
ongezeko la ukusanyaji mapato ya Serikali," amesema Waziri Dkt.
Mwigulu.
Amebainisha kuwa tume hiyo itanza
kufanya tathimini kwenye mifumo ya ukusanyaji mapato na kwamba
itakapomaliza itahamia kwenye mngine ikiwemo tathmini ya ukuaji na
ugharimiaji wa deni laSerikali, ulipaji wa mishahara, malimbikizo ya
madeni na ukuaji wake.
Amesisitiza kuwa uchumi
wa nchi unakua kwa asilimia 6.4% hali iliyosababisha nchi kufikia hadhi
ya uchumi wa kati kwani kiwango hicho cha uchumi kinatatarajiwa
kiendane na ukusanyaji wa mapato.
Ameongeza
kuwa wastani wa Nchi za Jumuiya ya Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC)
ukusanyaji wa mapato huchangia asilimia 15.1% ya pato la taifa huku
zilizoendelea hupata asilimia 40% ya pato hilo kuzifanya kuweza
kugharamia miradi ya maendeleo.
Kwa upande wake
Mjumbe wa Tume hiyo Profesa Nehemiah Usoro amesema watahakikisha
wanatekeleza majukumu yao ili kufanikisha malengo yaliyowekwa katika
kuboresha mifumo ya mapato na matumizi ya Serikali..
Tume
hiyo inaundwa na wajumbe 10 ikiongozwa na Mwenyekiti wake Profesa
Samweli Wangwe itafanya kazi kwa muda wa miezi sita kuanzia Agosti 25
mwaka huu.
No comments:
Post a Comment