Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Timu
ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania 'Twiga Stars' imempongeza na
kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwa mlezi na mfadhili
wa timu hiyo katika mashindano mbalimbali huku ikimuahidi kufanya
makubwa katika michuano itakayoshiriki.
Hatua
hiyo imekuja siku chache wakati baada ya Rais Samia akiipongeza Timu ya
Taifa ya Vijana (U-20) iliyotwaa ubingwa wa CECAFA alitoa kauli ya
kuahidi kudhamini mashindano hayo kwa wanawake yatakayofanyika mwakani.
Pongezi
na shukrani hizo zimetolewa leo jijini Dar es Salaam na wachezaji wa
timu hiyo wakati wakizungumza na wanahabari jijini humo.
Mchezaji
wa Twiga Stars Ester Mabanza amesema wanampongeza na kumshukuru Rais
Samia kwa kuwa amekuwa mstari wa mbele kuisaidia timu hiyo tangu akiwa
Makamu wa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano hivyo kupitia yeye italeta
chachu ya kuendeleza soka la wanawake.
"
Napenda kumshukuru Rais Samia kwa kutusaidia amekuwa nasi tangu hajapata
urais ametupa sapoti katika mashindano tuliyoshiriki na kutupa moyo wa
kuendelea kupambana kufikia malengo," amesesma Ester.
Amebainisha
kuwa Rais Samia kwao ni mama, mlezi na mkuu wa nchi na kwamba
wataendelea kupokea ushauri wake na kushirikiana naye kufannikisha
malengo yao waliyojiwekea.
Kwa upande wake
Mchezaji, Janenth Christopher amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea
kulipigania soka la wanawake kwani amekuwa nao bega kwa bega katika
kuwasaidia na kuwafadhili na kwamba wanamuahidi kufanya vizuri katika
mashindano yaliyo mbeleni mwao.
Amewaomba wadau
wa soka kujitokeza kuunga mkono juhudi za Rais Samia ikiwemo kuisaidia
timu hiyo kupata wadhamini wengine, kulitangaza soka la wanawake pamoja
na uboreshaji wa miundo y a mchezo huo kwani itasaidia kupata timu bora
ya taifa.
Mchezaji huyo ameawomba wadau wa soka
wasichukulie kauli ya Rais Samia kwa mtazamo hasi kwani Rais alisema
wachezaji wa kike kujiweka kama wanaume imechukuliwa tofauti kwani
aliitoa katika kuwafunza na wataitumia kuendeleza mapambano.
Ametoa
rai kwa wazazi na walezi wenye watoto wa kike wenye vipaji vya soka
kuwapa moyo na kuwaendeleza watoto wao ili kufanikisha timu bora za
wanawake bora za wanawake katika ngazi za vilabu na taifa.
Naye
Stumai Abdallah amesema mchezo wa soka unahitaji mtu kuwa na nguvu ndio
maana wanafanya mazoezi kujiweka imara hivyo wtau wasiwachukulie kiume
na kumuahidi Rais Samia kufanya vizuri katika mashindano
Mjumbe
wa Kamati ya Utendaji wa Chama cha Mpira Wanawake Tanzania (TWFA) Zena
Chande amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuwa mlezi wa Twiga Stars na
kwamba ameonyesha nia ya dhati kuidhamini timu hiyo kufikia malengo.
No comments:
Post a Comment