Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mji, Silvestry Koka, akikabidhi madawati kwa baadhi ya shule zilizopo katika jimboni kwake.
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Mbuge
wa Jimbo la Kibaha mji Silvestry Koka katika kuunga mkono juhudi za
serikali katika kuboresha sekta ya elimu ameamua kuchangia madawati
yapatayo 120 kwa shule za msingi na sekondari.
Koka
amekabidhi msaada huo wa madawati na viti kwa shule tatu za sekondari
na moja shule ya msingi muungano ambayo ilipatwa na janga la kuungua na
Moto hivi karibuni.
Mbunge
huyo ambaye katika ziara hiyo ambayo iliweza kugusa zaidi katika sekta
ya elimu aliambatana na wajumbe wa mfuko wa Jimbo pamoja na baadhi ya
viongozi wa idara za elimu kutoka halmashauri ya mji Kibaha.
Katika
ziara hiyo Mbunge huyo Alisema kuwa lengo lakek kubwa kwa Sasa ni
kuweka mikakati kabambe kwa ajili ya kuzisaidia shule za msingi na
sekondari zilizopo pembozoni ili nazo ziweze kufanya vizuri.
"Kwa
upande wangu mm Kama Mbunge wa Jimbo la Kibaha mji kipaumbele changu
kikubwa kwa Sasa nitatumia fedha za mfuko wa Jimbo Kama asilimia 70 kwa
lengo la kuboresha elimu,"Alisema Koka.
Aidha alifafanua kwamba lengo la serikali ya awamu ya sita ni
kuhakikisha inaboresha zaidi mazingira rafik kwa wanafunzi pamoja na
walimu ili kuleta mabadiliko zaidi katika kuongeza kiwango Cha elimu.
Pia
alisema anatambua bado kuna baadhi ya shule katika Jimbo lake
zinakabiliwa na changamoto mbali mbali hivyo atajitahidi kwa Hali na
mali kuzisikiliza na kuzitafutia ufumbuzi kwa kushirikiana na serikali
na wadau wadau wa maendeleo.
Aliongeza
kuwa ana Imani mchango wa madawati hayo pamoja na viti vitawasaidia
wanafunzi kwa kiasi kikubwa kusoma katika mazingira mazuri ukilinganisha
na siku za hapo nyuma.
Katika
hatua nyingine aliwakumbusha wanafunzi kuhakikisha wanasoma kwa bidiiii
na kusikiliza Yale yote ambayo yanafundishwa na walimu wao.
Mbunge
huyo kupitia ziara hiyo aliwaahidi walimu na wanafunzi kuendelea
kutatua changamoto za uhaba wa matundu ya vyoo pamoja na upungufu wa
madarasa na nyumba za walimu.
Kwa
upande wake Diwani wa Kata ya Mkuza Fokasi Bundala alimpongeza Mbunge
huyo kwa juhudi ambazo anazifanya kwa kuboresha sekta ya elimu kupitia
fedha za mfuko wa Jimbo.
Nao
baadhi ya wanafunzi na walimu ambao shule zao zimeweza kunufaika na
msaada huo wamesema kwamba madawati hayo yatatakuwa no mkombozi mkubwa
katika suala zima la kuindokana na kusoma kwa mlundikano mkubwa.
Katika
ziara ya jumla ya madawati yapatayo 120 yamekabidhiwa kwa shule ya
Sekondari nyumbu,Simbani,Mbwawa pamoja na shule ya msingi Muungano kwa
kiasi Cha shilingi milioni 78 fedha kutoka mfuko wa Jimbo.
No comments:
Post a Comment