Sehemu ya wananchi wakifanya usafi katika Kata ya Mushasha Kijiji Bulembo eneo mahususi kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya.
Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Kanali Wilson Sakulo akiwahimiza wananchi kuchangamkia fulsa ili kujikomboa kiuchumi.
Na Lydia Lugakila, Misenyi Kagera
Baada ya kilio cha muda mrefu kwa wananchi wa kata za Kyaka, Mushasha wilayani Misenyi mkoani Kagera kutembea umbali mrefu kwa zaidi ya kilometa 50 kufuata huduma ya afya katika hospitali ya Mugana hatimaye kiu ya uhitaji wa huduma hiyo imekata ni baada ya ujenzi huo kutarajiwa kuanza muda wowote kuanzia Sasa.
Wakiwa eneo la Kijiji Bulembo kata Mushasha eneo inapojengwa hospitali hiyo katika zoezi la usafi kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi, wananchi hao akiwemo Revocatus Babeiya na mzee John Karwani Mbyazita wameishukuru serikali kupitia mbunge wa jimbo la Nkenge wilayani humo Frolent Kyombo, kwa kuendelea kupaza sauti akiwa bungeni juu ya kilio hicho cha kujengewa hospitali ya wilaya wameshukuru kuona shilingi milioni 500 zimeishaletwa wilayani humo tayari kwa kuanza na vyumba 2 vya mwanzo ambavyo ni chumba cha utawala na mahabara vinavyotarajiwa kuanza kujengwa.
Wananchi hao ambao wamejitolea eneo hilo lenye ukubwa wa hekali 40 wameeleza kupokea huduma hiyo kwa furaha sana kuwa wako tayari kuwekeza nguvu kubwa ikiwa ni pamoja na kutoa ushirikiano kwa serikali ili kufanikisha ujenzi huo.
Akizungumzia hatua hiyo mbunge wa jimbo la Nkenge wilayani Misenyi Frolent Kyombo amewapongeza wananchi hao waliojitokeza katika shughuli ya usafi, viongozi wa wilaya hiyo huku akiwataka wananchi kuhakikisha kuwa fedha za serikali zinapoletwa waongeze nguvu ili kufanikisha malengo kuzudiwa.
"Katika ilani ya uchaguzi serikali iliainisha ndani ya kipindi cha miaka 5 kuwa hospitali 98 zitajengwa mojawapo ikiwa ni wilaya ya Misenyi na ndani ya kipindi hiki, tunaamini kwamba hispitali itakamilika kwa majengo yake sasa tumeanza kwa kasi kubwa kwa kupata Milioni 500 kabla ya miaka 5 kuisha ujenzi wa hospitali utakuwa umekamilika.
Kyombo amewahimiza wananchi wilayani humo kuhakikisha wanalinda raslimali zote zitakazoletwa kwa ajili ya ujenzi huo huku akiwataka viongozi wa chama na serikali kuhakikisha vijana Katika maeneo hayo wanashiriki katika ujenzi ili kupata ajira na kipato.
Ameongeza kuwa wilaya ya Misenyi ina vituo vya afya 2 ambavyo ni Bunazi na Kabyaile ambapo pia katika bajeti ya mwaka wa fedha 2021-2022 kupitia maelekezo ya Tamisemi bajeti ya halmashauri wanao ujenzi wa kituo cha afya kimoja ambapo kikipatikana kitakuwa maeneo ya Kanyigo hivyo anaamini ndani ya miaka 5 katika maeneo mengi huduma za afya zitaendelea kuboreshwa hivyo kuwasihi wananchi kuendelea kushirikiana na serikali kuliko kusubiri kuletewa.
Aidha kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Misenyi kanali Wilson Sakulo ameishukuru serikali kukata kiu ya wananchi na kuamua kutoa kiasi hicho cha fedha na kuwaondolea wananchi changamoto iliyokuwepo, huku akiagiza ratiba za ujenzi kuendelea na kuwahimiza wananchi kuchangamkia fulsa ili kujikomboa kiuchumi.
Naye Innocent Mkandala Mkurugenzi wa halmashauri hiyo amemshukuru mbunge wa jimbo la Nkenge kwa kufuatilia kila mara na kuwasemea wananchi hao na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha hadi kukamilika kwa ujenzi huo.
Kwa upande wake mganga mkuu wa wilaya hiyo Edward Kagari amesema baada ya kukamilika majengo hayo 2 wataendelea na majengo yanayofuata kulingana na fedha watakazopokea toka serikalini kwani uhitaji ni vyumba 26 hadi kukamilika kwa hospitali hiyo huku makadilio yakiwa ni bilioni1.
" Hospitali hii inatarajia kuhudumia vijiji 77vilivyopo katika halmashauri yetu na inatarajia kuwahudumia wananchi takribani laki 2, 76 elfu 908 ikiwemo huduma za msingi za mama na mtoto ambapo majengo hayo 2 tunatarajia kukamilika ifikapo mwezi octoba mwaka huu" alisema Kagari
Hata hivyo kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Projectus Tegamaisho ameishukuru serikali kwa kukubali kuwapatia hospitali ya wilaya na kumshukuru diwani wa kata ya Mushasha Oscar Nestor kupitia Kijiji Bulembo waliojitokeza ardhi hiyo bure na kuongeza kuwa kupitia mapato ya ndani halmashauri hiyo itazidi kutenga ili kuhakikisha hospitali inajengwa na kuisha haraka na kuanza kutumika.
No comments:
Post a Comment