Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Shirika
la Utangazaji Tanzania (TBC) limesaini Mkataba wa Haki za Matangaza ya
kutangaza Mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara redioni wenye thamani ya Sh
Bilioni 3.54 na Shirikisho la Soka Nchini (TFF) kwa kipindi cha miaka
10.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es
Salaam katika hafla ya utiaji saini mkataba huo Mratibu wa Miradi na
Masoko wa shirika hilo, Gabriel Nderumaki amesema wameamua kusaini
mkataba kuendelea kuipa hadhi na thamani ligi pamoja na kuvisaidia
vilabu kuviondolea changamoto katika mashindano hayo.
Amebainisha
kuwa TBC wameiona fursa ya kutangaza ligi hiyo lengo likiwa kuipaisha
ifike kuwa miongoni mwa ligi bora na kwamba uingiaji mkataba huo ni
chachu ya maendeleo ya soka katika Mashindano ya Ligi hiyo.
Kwa
upande wake Rais wa TFF , Wallace Karia amelishukuru shirika hilo kwa
kuonyesha ni kwa jinsi linatambua umuhimu pamoja na dhamira ya kuendelea
kuipa thamani ligi kuu na kwamba mkataba utasaidia kupunguza
changamoto za vilabu vinavyoshiriki ligi hiyo.
"
Miaka nyuma suala halikuwepo ila kwa sasa inaonyesha jinsi ligi yetu
inavyoendelea kupanda thamani siku hadi siku mkataba huu ni ukombozi kwa
vilabu katika kuvipunguzia makali ya uendeshaji wakati wa mashindano,"
amesema Karia.
Amesisitiza kuwa wakati TFF
inaanza utiaji mikataba ya kuipa thamani ligi vilabu vishiriki vilikuwa
vipkipatiwa Sh Milioni saba ikaongezeka kwa udahamini wa matangazo ya
Televisheni kufikia Sh milioni 100 na kwamba kwa msimu ujao utafiki Sh
mil 400.
Ameongeza kuwa mkataba huo hauzizuii
redio nyingine kutangaza ligi hiyo bali zinatakiwa kuingia makubaliano
na TBC lenye mkataba wa kutangaza matangazo redioni na kukazia duniani
kote mkataba wa aina husainiwa kwa nuda mrefu sababu mwekezaji hununua
mitambo mipya hivyo huhitaji kurudisha gharama na kupata faida.
Amefafanua
kuwa TFF limeanza kupata fedha kupitia mitandao yake ikiwemo Runinga ya
Ligi kuu pamoja na mitandao ya kijamii ya Instagram, na kubainisha
fedha zinakuja kutokana shirikisho kuwa imara kiutendaji.
Naye
Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Salum Madadi amelishukuru TBC na
kusema mkataba huo utatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya soka kwa
kuifanya ligi kuwa bora na yenye thamani.
Mwenyekiti
wa Klabu ya Mbeya City, Venance Msolla amesema ili vilabu viwe bora na
viweze kujiendesha vinahitaji benchi bora la ufaundi, usajili wa
wachezaji wazuri na kwamba mkataba utazisaidia timu za mikoani
kuondokana na changamoto za kiundeshaji.
No comments:
Post a Comment