HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 27, 2021

JWT yampongeza Rais Samia Hassan Suluhu kwa agizo la kuondolewa Machinga

 

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), Abdallah Mwinyi akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kwa niaba ya uongozi wa jumuiya hiyo.

 

Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam

JUMUIYA ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), imempongeza Rais Samia Hassan Suluhu na serikali yake  kwa  kuagiza wafanyabiashara wadogo (Machinga), kuondolewa mbele ya maduka.

Haya yalisemwa jana na Katibu Mkuu wa JWT kwa niaba ya uongozi wa jumuiya hiyo Abdallah  Mwinyi alisema kitendo cha  Machinga kukaa mbele ya maduka ya  Wafanyabiashara walio rasmi kilifilisi mitaji ya wafanyabiashara hao.

Mwinyi alisema agizo hilo la Rais Samia ni ukombozi mpya kwa wafanyabiashara na makusanyo ya kodi kwa Taifa na kwamba wanatambua  kuna baadhi ya wafanyabiashara walitumia fursa ya mpangilio holele wa Machinga kukwepa kodi.

" Tunampongeza Rais kwa kubaini tatizo hili na kutoa muongozo sahihi wenye usawa katika haki kwenye mazingira ya biashara. Sisi kama jumuiya ya wafanyabiashara tunampongeza na hii itasaidia kuwarejesha walioende kuwekeza biashara zao nchi za jirani," alisema Mwinyi.

Katibu huyo aliongeza kuwa mara kadhaa Rais Samia wakati akiwaapisha wateule wake amekuwa akiagiza kuhakikisha viongozi wote wanaboresha mazingira ya biashara ikiwamo wafanyabiashara kutokusanyaswa.

Pia alisema kuwa Rais Samia alienda mbali zaidi kwa kumuelekeza Waziri wa Fedha na Mipango Nwigulu Nchemba kuhakikisha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), inasimamia sheria bila kutumia mabavu na kukataa kodi za dhuluma.

"Jambo hili limewafariji wafanyabiashara ambao walikata tamaa kutokana na kipindi cha nyuma kufanyiwa mahesabu yasiyoendana na vipato vyao hali iliyosababisha wengi kustakiwa kwa makosa ya kuhujumu uchumi baada ya kuingia makubaliano na kushindwa kulipa kodi hii," alisema Mwinyi.

Aliongeza kuwa hali hiyo  iliwavunja moyo na  wengi wao kulazimika kutafuta namna ya kunusuru mitaji yao.

Alisema kuwapo kwa Machinga mbele ya maduka ya wafanyabiashara hao kilisababisha wengi kufilisika na wengine kuhamia nchi jirani kufanyabiashara jambo ambalo linaikosesha Tanzania kupata Kodi.

Aidha jumuiya hiyo inashauri kabla ya kuruhusu mradi wa ujenzi wa kituo kikubwa cha biahsra Ubungo ni vema likafanyika kongamano  kubwa la uhuru wa maoni kwa wadau na waagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi ili kuepusha Watanzania kuwa watumwa wa biashara kwenye soko la ndani.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa JWT   Staphen Chamle  alisema msimamo na mtazamo wa jumuiya hiyo walitaka Machinga hao kutengewa maeneo yao ili wasiingiliane na wafanyabiashara walio rasmi lengo ni  kuondoa mgongano wa maslahi.

"Haiwezekanii mtu aliyepanga fremu analipa kodi zote kuna tofauti kubwa anayelipa kitambulisho cha 20,000 kwa mwaka na  bidhaa ni ile ile kwa kuwa Machinga halipi kodi atauza kwa bei anayotaka," alisema Chamle.

No comments:

Post a Comment

Pages