Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Serikali
imesema itaendelea kutoa mafunzo ya ufundi kwa vijana nchi nzima ili
kukabiliana na tatizo la ajira huku ikibainisha takwimu zinaonyesha
mahitaji ya vijana ianaongezeka siku hadi siku na kwamba asilimia 31.5%
ya watu waliopo nchini ni vijana sawa na asilimia 57% ya nguvu ngazi ya
taifa.
Hayo
yamesemwa jijini Dar es Salaam na Ofisa Maendeleo ya Vijana Mkuu kutoka
Ofisi ya Waziri Mkuu( Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Ofisa Maendeleo ya Vijana Mkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Julius Tweneshe
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa kikao cha Vijana kuthibitisha Rasimu ya Sera ya
maendeleo ya taifa jijini Dar es Salaam Mwakilishi kutoka ofisi ya
Waziri Mkuu bw. Julias Tweneshe alisema takwimu zinaonyesha kuwa Hali
ya mahitaji ya vijana nchini imekuwa ikiongezeka siku Hadi siku ambapo
asilimia 31.5 ya watu waliopo nchini ni vijana Sawa na Asilimia 57 ya
nguvu kazi ya Taifa.
"Serikali
Katika Kuhakikisha kundi hili linapewa kipaumbele kuweza kuchangia
Uchumi wa nchi Serikali imeunda sera vijana ya Mwaka 1996 inayo wahiza
vijana kujitolea" Alisema bw Tweneshe.
Alisema katika Marekebisho ya sera hiyo iliyofanyika 2007 sera hiyo ililenga kitenga Maeneo Maalumu ya kiuchumi kwa vijana.
Tweneshe
aliongeza kiwa katika Kuhakikisha masuala ya vijana yanazingatiwa
Serikali Imetenga Asilimia 10 kwa ajili ya mikopo kwa vijana kwa kila
halmashauri ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.
Aliongeza kuwa katika sera Mwaka huu imelenga kutatua changamoto za kukuza ujuzi kwa ngazi kitaifa na kimataifa.
Naye
Mkurugenzi wa community Harb Foundation, Paul Makoe amesema rasmu ya
awali ni tofauti na Mwaka huu ambayo imeongezewa vipengele vya watu
wenye ulemavu na ajira zimeanza kuwainua vijana.
No comments:
Post a Comment