Mkurugenzi wa Taasisi ya Mulika Tanzania Bw. Hussein Melele akiwasilisha hoja wakati wa kikao cha vijana cha Kupitia na Kuthibitisha Rasimu ya Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana Jijini Da r es Salaam.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Serikali
imesema itaendelea kutoa mafunzo ya ufundi kwa vijana nchi nzima ili
kukabiliana na tatizo la ajira huku ikibainisha takwimu zinaonyesha
mahitaji ya vijana inaongezeka siku hadi siku na kwamba asilimia 31.5%
ya watu waliopo nchini ni vijana sawa na asilimia 57% ya nguvu ngazi ya
taifa.
Hayo
yamesemwa jijini Dar es Salaam na Ofisa Maendeleo ya Vijana Mkuu kutoka
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye
Ulemavu Julius Tweneshe katika Kikao cha kujadili Rasimu ya Taifa ya
Maendeleo ya Vijana kilichofanyika Ukumbi wa Karimjee kikiwakutanisha
vijana kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Pwani na Tanga.
Amesema
kuwa Serikali ina dhamira kukabiliana na changamoto ya ajira hivyo
mafunzo yanayoendelea kutolewa kwa vijana yatawasaidia kuweza kujiajiri
katika sekta mbalimbali
"Serikali
katika kuhakikisha kundi hili linapewa kipaumbele kuweza kuchangia
Uchumi wa nchi Serikali imeunda sera vijana ya Mwaka 1996 inayo wahiza
vijana kujitolea" amaesema Tweneshe.
Amebainisha
kuwa katika Marekebisho ya sera hiyo iliyofanyika 2007 sera hiyo
ililenga kutenga maeneo maalumu ya kiuchumi kwa vijana.
Amesisitiza
kuwa kiwa katika kuhakikisha masuala ya vijana yanazingatiwa Serikali
imetenga asilimia 10% kwa ajili ya mikopo kwa vijana kwa kila
halmashauri ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.
Ameongeza kuwa katika sera mwaka huu imelenga kutatua changamoto za kukuza ujuzi kwa ngazi kitaifa na kimataifa.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa community Harb Foundation, Paul Makoe amesema
rasmu ya awali ni tofauti na waka huu ambayo imeongezewa vipengele vya
watu wenye ulemavu na ajira zimeanza kuwainua vijana.
Nae
Kijana Tatu Sultan mwenye ulemavu wa ngozi amependekeza kuwa vijana
wenye makundi maalum wapewe kipaumbele katika masuala mbalimbali
yakiwemo masuala ya ajira ili kuondokana na vitendo vinavyashiria
unyanyapaa kwa jamii inayowazunguka.
No comments:
Post a Comment