Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Tanzania
imeokea msaada wa Euro milioni 25 sawa na Sh Bilioni 67.82 kutoka
Serikali ya Ujerumani kupita Benki yake ya Maendeleo ya KfW, kwa ajili
ya Mradi wa Uhifadhi Endelevu wa Maliasili na Mifumo ya Ikolojia.
Mkataba
wa msaada huo umesainiwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Emmanuel Tutuba,
kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo
ya Ujerumani wa Umoja wa Afrika Christoph Tskens, kwa niaa ya Serikali
ya Ujerumani.
Akizungumza katika hafala utiaji
saini mkataba huo Katibu Mkuu huyo amesema kuwa fedhaizo ziatatumika kwa
ajili ya kuendeleza na kuhifadhi maliasili katika Hifadhi ya Serengeti
pamoja na kugharamia mradi wa uhifadh endelevu wa maliasili na mifumo ya
Ikolojia katika maeneo ya Ushoroba wa Katavi-Mahale.
"
Lengo la mrdai wa Serengeti ni kuchnagia maendeleo ya kijamii,
kiuchumi, na usimamizi endelevu wa maliasili katika Wilaya ya Bariadi,
Bunda, Serengeti, na Ngorongoro wakati wa mradi wa Ushoroba wa
Katavi-Mahale unalenga usimamizi wa maliasili sambamba na kuboresha
maisha ya wananchi kwa kuhusisha matumizi bora ya ardhi na utoaji wa
hatimiliki za kimila," amesema Tububa.
Amebainisha
kuwa kiasi cha Sh Bilioni 21.7 zitatumika katika mradi wa kuendeleza a
kuhifadhi maliasili katika hifadhi ya Serengeti na Sh Bilioni 46.12,
zitaenda kwenye mradi wa uhifadhi endelevu wa maliasili na mifumo ya
Ikolojia ushoroba wa Katavi- Mahale.
Kwa upande
wake, Blozi wa Ujerumani nchini tTanzania, Regine Hess ameahidi kuwa
nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuboreshamazingira
ili kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya nchi ambayo hayaiathiri
Tanzania pekee bali duni akwa ujumla.
Nae
Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani wa Umoja wa Afrika,
Tiskens amesema kuwa benki hiyo itaendelea kuisaidia Tanzania katika
sekta ya utalii kwa kuboresha maeneo ya uhifadhi pamoja na kuziweezsha
jamii zinazozunguka maeneo hayo li waweze kuzitunza hifadhi hizo.
Tanzania
imekuwa ikinufaika na ufadhili wa Serikali ya Ujerumani katika sekta za
afya, maji, nishati, matumizi endelevu ya maliasili na usimamizi bora
wa fedha za umma amabpo kiasi cha Sh Bilioni 678.54 zilitolewa kwa ajili
ya miradi inayoendelea kutekelezwa na shilingi Bilioni 599.23 kwa
miradi iliyokamilika.
No comments:
Post a Comment