Rais wa TCCIA, Paul Koyi, akimtambulisha Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa chemba hiyo Judith Karangi katika kikao cha Menejimenti, kushoto ni Mjumbe wa bodi wa TCCIA, Dkt. Said Kingu.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Chemba
ya Wafanyabiashara wenye Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) imesaini
hati ya makubaliano ya ushirikiano na taasisi tatu ili kuwawezesha
wazawa kushiriki kikamilifu katika miradi ya kimkakati inayotekelezwa
nchini pamoja na kuwaondolea changamoto mbalimbali wafayabiashara.
Miongoni mwa miradi hiyo ni Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACop) pamoja na Mradi wa Gesi Asilia.
TCCIA
imeingia makubaliano hayo na Jumuiya ya Watoa Huduma katika Sekta ya
Mafuta na Gesi Asilia Tanzania (ATOGs), Shirikisho la Wafanyabiashara
na Wenye Viwanda wa Zanzibar (ZNCCIA) na Saccos ya Wanawake
Wajasiriamali Nchini (TASWE).
Akizungumza
jijini Dar es Salaam katika Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo Rais
wa TCCIA Paul Koyi amesema wenye viwanda na wafanyabiashara na
wanachama na taasisi zilizohusika zitapiga hatua kimaendeleo na
changamoto zinazowakabili zitatuliwa kwa urahisi.
"
Tumekuwa na tukishirikiana kabla ya makubaliano haya tunaamini yataenda
kutatua changamoto za wafanyabiashara wa Tanzania Bara na Visiwani
hivyo yatakuza biashara na viwanda kiuchumi," amesema Koyi.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya ATOGs, Abdulsamad Abdulrahim
makubaliano hayo yatasaidia wazawa kushirikishwa na kupata fursa kutoa
huduma pamoja na kuudha bidhaa zinazotengenezwa nchini.
Nae
Mwanzilishi wa TASWE, Anne Matinde amese,ma matarajio ya wanachama
anawaongoza kuwa huru katika utekelezaji wa majukumu yao hasa pale
wanapokutana na wateja wa mataifa ya nje juu ya bidhaa zao.
Katika
hatua nyingine imepata Mkurugenzi Mtendaji Mpya ambaye ni Judith
Karangi na kwamba ameahidi kuifanyia marekebisho taasisi hiyo sambamba
na kuwaleta pamoja wadau waote wa sekta hizo.
Akizungumza
baada ya kutambulishwa na Rais wa chemba hiyo, Judith ameihakikisha
bodi ya wakurugenzi na wafanyakazi kuwa atafanya kazi kwa bidii na
weledi ikiwemo kurejesha imani kwa wafanyabiashara wote nchini.
Akimtambulisha
mkurugenzi mtendaji huyo, Rais wa TCCIA, Koyi amesema ana imai kubwa
pamoja na bodi hiyo ataipaisha chemba hiyo kutoka ilipo na kusomba mbele
zaidi hivyo aliwaomba wafanyakazi kumpa ushirikiano kwani mafanikio ya
taasisi hiyo yatategemeana na umoja na mshikamano katika utendaji kazi.
Nae,
Mjumbe wa Bodi ya TCCIA, Dkt. Said Kingu amewataka wadau sekta zote na
kumpa ushirikiano mkurugenzi huyo kwa kuwa ni mtu mzoefu kweny utendaji
kazi na kuongeza kuwa taasisi hiyo ina nafasi kubwa ya kutimiza malengo
ya Serikali ya kuimarisha uchumi.
No comments:
Post a Comment