Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza katika uzinduzi wa vituo vya Huduma Pamoja uliofanyika katika Viwanja vya Shirika Posta Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Posta.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amezindua Vituo vya Huduma Pamoja (One Stop
Centre Services) vya Shirika la Posta Tanzania(TPC) na kuziagiza taasisi
za umma ambazo hazijaanza kutumia huduma za vituo hivyo kuanza kutoa
huduma katika vituo vinavyopatikana ndani ya shirika hilo katika mwaka
wa fedha wa 2021/22.
Maagizo hayo ameyatoa leo
jijini Dar es Salaam katika Hafla ya uzinduzi wa vituo hivyo na
kubainisha kuwa ni sehemu ya utekelezaji ya Maelekezo ya Rais Samia
Suluhu Hassan inayoakisi Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka
2020 na kwamba lengo la Serikali kuona mchango wa sekta ya habri
mawasiliano unachangia uchumi pamoja na kuongeza ajira kwa wananchi huku
akizielekeza taasisi zinazotoa huduma kuweka vituo vya huduma kwenye
shirika hilo.
' Nazielkeza taasisi zinazotoa
huduma zijiunge na huduma hii Ofisi ya Rais na utumisi wa umma
hakikisheni taasisi zote zinajiunga na kuanza kutumia, vituo hivi
vitasaidia watu kuinua vipato na kuchocha maendeleo ya nchi," amesema
Waziri Majaliwa.
Amezitaja baadhi ya taasisi
hizo ni Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC), Mamlaka ya Dawa na Vifaa
Tiba,( TMDA ), Maeneo Maalum kwa Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA),
Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Shirika la
Viwango Tanzania (TBS), Tume ya Ajira na Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi.
Ametoa wito kwa wananchi
kujitokeza kwa wingi kupata huduma hiyo katika vituo vilivyoanza kazi
katika Ofisi Kuu za Posta za Dar es Salaan na Dodoma kwani kufanya hivyo
kutawapunguzia msongamano katika ofisi za taasisi pamoja na kuokoa
muda wa kupata huduma.
Amesisitiza kuwa
kuanzishwa vituo hivyo ni mageuzi makubwa ya shrika hilo lenye ofisi 350
nchi nzima hivyo na kwamba vitawapunguzia wananchi changamoto ya
kutembe ofisi ya taasisi zaidi ya moja kufuata huduma.
Waziri
Majaliwa amewasihi na kuwahimiza watumishi wa shirika la posta kufanya
kazi kwa weledi na kumpa ushirikiano Kaimu Postamasta Mkuu ili wafikie
malengo waliyojiwekea kuyatimiza.
Kwa upande
wake, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine
Ndungulile ameishukuru Serikali kwa kutoa Sh Bilioni 3.9 kwa ajili ya
kuboresha shirika hilo kwa mfumo wa kidijitali na kwamba watapokea fedha
nyingine Sh Bilioni 3.9 ambazo zitakwenda kuboresha mfumo huo.
Waziri
Dkt. Ndungullile amesema wizara hiyo imedhamiria kufanya mabadiliko
ndani ya shirika hilo hasa kwa katika mwonekano mpya, mwelekeo mpya
lengo likiwa kuifanya posta kuwa kitovu cha biashara.
Pia
amesema ifikapo mwaka 2025 kutakuwa na dirisha moja lenye huduma za
taasisi zote huku akiwaomba wanahabari na viongozi wakawe mabalozi wa
kuvitangaza vituo hivyo kwa jamii ifahamu kuwa posta imeshaaza kutoa
huduma ya vituo hivyo.
Naye Kaimu Postamasta
Mkuu, Macrice Mbodo amesema mradi wa vituo hivyo ni sehemu ya mradi ya
Tanzania ya Kidijitali na kwamba tayari Serikali imeshatenga Sh Bilioni
49.5 kuhakikisha unafika nchi nzima.
Kaimu
postamasta MKuu huyo amesema awamu ya kwanza inahusisha vituo 10 katika
mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Mbeya, Morogoro, Tanga, Mwaza,
Kigoma, Mjini Magharibi, na Pemba (Chake Chake).
Mbodo
amebainisha awamu ya pili ya vituo hivyo itaanza Januari 2023 na
kukamilika mwezi Juni mwaka 2024 ukihusisha kuuganishwa vituo 17 kwenye
dirisha moja kwenye mikoa ya Pwani, Iringa, Songwe, Rukwa,Njombe,
Kilimanajro, Tabora, Lindi, Kagera, Simiyu, Manyara, Katavi na Geita.
Pia
amefafanua kuwa awamu ya tatu ya vituo vya huduma pamoja itaanza mwezi
Julai 2024 na kukamilika mwaa 2025 huduma zitakuwa katika dirisha moja
kuwasaidia wananchi kupata urahisi na kutopeteza muda.
Amezitaja
huduma zilizoanza kutolewa katika Vituo vya Dar es Salaam na Dodoma ni
Utoaji wa Leseni za Biashara (TRA), usajili wa vifo na vizazi (RITA),
uhamiaji, usajili wa makampuni na majina ya biashara (BRELA),
Vitambulisho vya Taifa (NIDA), huduma za wastaafu (NSSF na PSSF) pamoja
na huduma za halmashauri.
Katika hatua nyingine
amesema wanajipanga kimkakati chini ya wizara husika kutelekeza
vipaumbele vinne kuimarisha eneo la usafirishaji wa mizigo na vifurushi,
uwakala na uuzaji wa fedha, biashara mtandao kupitia duka la mtandao na
posta kiganjani iatakayotoa fursa kwa mteja kufahamu mwenendo mzima wa
mzigo wake.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais, Utumishi na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael ameipongeza
Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuanzisha vituo hivyo kwani vitasaidia
utaoji wa huduma kwa watja wa shirika la posta na taasisi.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundo Mbinu Selemani Kakoso ameiomba
serikali kufuatilia deni la Sh Bilioni 3 la taasisi zinazodaiwa na posta
zilipwe ili shirika liweze kusimama kiundeshaji.
Katibu
Mkuu -Umoja wa Posta Afrika, Sifundo Moyo ameipongeza Serikali kwa
kufanya maboresho ndani ya shirika hilo hsa posta ya kidijitali hivyo
umoja huo utaendelea kushirikiana na Posta.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amempongeza Mbodo kwa uanzishaji
wa huduma za vituo hivyo na kubainisha kuwa vimekuja wakati mwafaka
hivyo ofisi ya mkoa itatoa ushirikiano kuhakikisha vinafanya kazi.
No comments:
Post a Comment