Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa tatu kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna wakizindua Asasi ya NMB Foundation yenye lengo la kuwekeza zaidi kwenye sekta ya elimu, mazingira, afya, kilimo na ujasiriamali, hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mwanaidi Ali Khamis na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NMB, Dk. Edwin Mhede. (Na Mpiga Picha Wetu).
NA MWANDISHI WETU
BENKI
ya NMB imezindua asasi ya kiraia iitwayo NMB Foundation, inayolenga
kujikita katika kuimarisha uwekezaji wake kwa jamii katika sekta tano
teule, sambamba na Mpango Maalum wa Udhamini wa Masomo 'NMB Nuru Yangu
Scholarship and Mentorship,' uzinduzi uliohudhuriwa na Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa.
Kupitia
NMB Foundation, benki hiyo inaunga mkono zaidi jitihada za Serikali
kuimarisha maendeleo, ambako inaenda kuvuka mipaka ya Programu ya
Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), ambayo kwa miaka 16 ya uwepo wake, imetumia
zaidi ya Sh. Bilioni 12 za urejeshaji kwa jamii kupitia asilimia moja
ya faida yake kila mwaka.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB (CEO), Ruth Zaipuna,
alisema asasi hiyo imejipanga kuacha alama kwa jamii ya Kitanzania,
kupitia uwekezaji na urejeshaji kwa jamii kwenye sekta tano za
kipaumbele ambazo ni elimu, afya, kilimo, mazingira na ujasiriamali.
Akichanganua
majukumu ya NMB Foundation, Zaipuna alisema katika elimu wanatarajia
kutoa misaada zaidi ya ilivyokuwa ikifanya kupitia CSR, ambako
itajielekeza kukuza elimu na kuongeza idadi ya watoto wanaopata elimu,
huku kwenye afya ikilenga kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa
makundi maalum na jamii kwa ujumla.
"Kwa
upande wa mazingira, tunakusudia kuhamasisha utunzaji wake kwa lengo la
kuboresha makazi ya jamii, wakati kwenye kilimo nia ni kuimarisha uwezo
wa vyama vya ushirika na kuwaongezea ujuzi kupitia elimu na mafunzo ya
masuala ya fedha, biashara na kuwajengea wakulima uwezo wa kukopesheka.
"Katika
ujasiriamali, NMB Foundation itahakikisha inafanikisha juhudi za
uzalishaji na utoaji ajira, lakini pia kukuza uchumi kwa kutoa mafunzo
na uwezeshaji wa elimu ya fedha, matumizi ya dijitali, ubunifu na
uendelezaji wa biashara ili kuharakisha mabadiliko chanya katika sekta
hiyo, inayokusanya Kundi kubwa la vijana," alisisitiza Zaipuna.
Kupitia
'NMB Nuru Yangu Scholarship and Mentorship,' Zaipuna alifafanua kuwa Ni
program ya ufadhili wa masomo kwa vijana wa ngazi ya chuo na Sekondari
wanaotoka katika familia zisizojiweza, ambao utaanzia mwaka huu wa
masomo wa 2021/22, wanakoratarajia kusaidia vijana 200, wakiwamo
wanachuo wa shahada ya kwanza 50 na wanafunzi wa Sekondari 150 kote
nchini.
Kabla ya kuzindua
NMB Foundation na NMB Nuru Yangu Scholarship, Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa aliipongeza NMB kwa ubunifu uliozaa asasi na program
zilizozinduliwa, ambazo ni rafiki kwa jamii, zinazoenda moja kwa moja
kusapoti jitihada za Serikali katika kusimamia maeneo yote yaliyotajwa
katika vipaumbele vitano vilivyoainishwa.
Alibainisha
kuwa, NMB sio wageni wa kuunga mkono jitihada za Serikali kutatua
changamoto za kijamii na kwamba NMB Foundation na NMB Nuru Yangu, ni
kielelezo cha benki inavyojitoa katika kuitendea haki jamii ya
Watanzania na kuwa kupitia CSR, kwa miaka mitano iliyopita benki hiyo
imeweza kuwafikia wanufaika zaidi ya milioni 5 kote nchini.
"UZINDUZI
huu unaofanyika hapa una baraka zote za Serikali, kwa sababu tunatambua
kuwa asasi hii ni muhimu kwa ustawi na maendeleo ya Taifa na watu wake,
kama ilivyo pia kwa Programu ya NMB Nuru Yangu, ambayo inaenda kuwabeba
mamia ya vijana wetu kutoka katika jamii ya wasiojiweza, ambao sisi
Kama Serikali tayari tumeshawekeza vya kutosha katika kuwakomboa
kielimu.
"Serikali tunaahidi sapoti ya kila namna kwa NMB kutokana na jinsi inavyojitoa katika kutuunga mkono kwenye maeneo mbalimbali.
"Mchango
wa NMB kwa jamii ni mkubwa unaopaswa kuigwa na wadau wengine. Serikali
inatambua na kuthamini harakati chanya za benki hii, tunawaomba
endeleeni kuchapa kazi, tuko nyuma yenu," alisisitiza Waziri Mkuu.
No comments:
Post a Comment