HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 30, 2021

DAR ES SALAAM DERBY' NI YANGA AMA AZAM LEO?

 

Kikosi cha Yanga.

 


Na John Marwa

Siku adhimu katika tasnia ya Soka la Tanzania. Ni Yanga na Azam ndani ya dakika 90, sekunde 5400 katika Nyasi za Dimba la Benjamin Mkapa pale kwa DC mrembo Jokate Mwegelo, Temeke.

Ni miongoni mwa mafahali watatu ndani ya NBC Premier League (NPL) 2021/22, mzunguko wa nne.

Yanga vinara wa NPL, mechi tatu point 9 clean sheet tatu ni ishara tosha kuwa wameanza katika gia sahihi msimu huu ukiondoa misimu minne iliyopita.

Ubora wa Yanga unaanzia langoni, safu ya ulinzi na safu ya kiungo,,, uimara wao uko kwenye pressing yao chini ya Fiston Mayele, Youcuba Sogne, Feisal Salum, Faridi Mussa hapa ndio kuna point tatu za Yanga katika Kila mchezo.

Azam FC licha ya kuanza vibaya msimu huu bado Kikosi chao kinatishia sana wapinzani wake, kutolewa CAF CC na Pyramid kumeonysha ukomavu wa Azam katika maeneo mawili, safu ya ulinzi na kiungo ni sehemu ambazo zinaimarika sana.

Sospeter Bajan ameonyesha uimara wa kukata njia za wapinzani kujidai katikati mwa Uwanja. Nado, Lyanga katika mapana ya kiwanja yanawafanya Azam kuwa hatari sana katika mikimbio na utengenezaji nafasi.

Ni wazi tunaenda kushuhudia kandanda safi sana kutoka Kwa Makocha wa pande zote mbili, uimara na utimamu wa kifikra kwa wachezaji wa timu zote utatoa upendeleo wa kuibuka na matokeo.

Sotarajii kushuhudia bao la mapema na kama litatokea sio kwa makosa ya kulazimishwa aidha mpira uliokufa ama wa kutenga.

Kama mchezo huu utafika dakika 30 bado hakuna bao basi kipindi Cha kwanza hakitakuwa na bao ama mabao.

Mwisho game itaishia hapa atakayekuwa vizuri kwenye pressing with actions, kwenye matukio ya probability actions na kusolve vyema mgawanyo wa wachezaji katika maeneo muhimu ya uwanja >> Matrix Equation kwa mfumo.

No comments:

Post a Comment

Pages