HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 30, 2021

WALIMU wapewe motisha kuongeza ufaulu

Na Lydia Lugakila, Bukoba


Katika kuendelea kuinua kiwango cha t
aaluma mkoani Kagera, imeshauriwa kuwapa walimu motisha kubwa pale wanapofanya vizuri kwa kuzingatia wao ndio wahusika wakuu katika ufaulu wa Wanafunzi.


Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Toba  Nguvilla wakati akichangia katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa Kagera, ambaye pamoja na Mambo mengine ameshauri kuwapa Walimu motisha itakayoacha alama badala ya Zawadi ya Bahasha kama ilivyozooleka.

Mhe. Nguvilla ameongeza kuwa Serikali Mkoa Kagera  kupitia Halmashauri ni vyema ikafikiria Sasa kuwapa Walimu wanaofaulisha Vizuri wanafunzi kwa Kuwapa Viwanja, Viwanja ambavyo baadae Walimu hao Wanaweza kujenga Nyumba zao, na itapelekea Walimu hao kutokuwa na mawazo ya kuhama maeneo yao ya Kazi.

Hayo yanajiri wakati ambapo kitakwimu Mkoa wa Kagera umeendelea kufanya Vizuri Mwaka hadi Mwaka, huku 2020 Mkoa ukipata Daraja A matokeo ya Jumla Mitihani yote ya Kitaifa.
[15:24, 10/30/2021] Bukoba Lydia: Mpaka wa Murongo uliopo Wilaya ya Kyerwa Mkoani  Kagera ni moja ya Chanzo kikubwa cha mapato endapo kitapewa kipaumbele na kuboreshwa katika muktadha wa fursa za Kiuchumi.

Mbali ya kuwa Mpaka huo kwa Sasa unaendelea na shughuli za Kawaida za kuvusha Wageni kutoka Nje ya Nchi pamoja na Magari yakiwemo Magari ya Mizigo, imebainika kuwa endapo mpaka huo utaboreshwa Kama kwingine, inaweza kuwa Fursa kwa Wakazi wa eneo husika pamoja na Chanzo Cha Pato la Mkoa na Taifa.

Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Rashid Mwaim ni moja ya wanaotamani kuona Mpaka wa Kyerwa ukiboreshwa kulingana na Hali ya Kijiografia ya Nchi Tatu zinazotumia Mpaka huo ikiwemo Uganda, DRC Congo na Sudani, hivyo maboresho yangefanyika katika nyanja ya miundombinu ikiwemo Barabara, Ujenzi wa Vitega uchumi ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa Bandari kavu itakayosaidia kupunguza Mizigo na Magari yanayopita mpaka wa Mutukula Wilayani Missenyi, kwa kufanya hivyo kuchangamsha uchumi.

No comments:

Post a Comment

Pages