HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 29, 2021

PRST chawataka Maafisa Uhusiano kutekeleza majukumu yao kwa niaba ya taasisi.

 


Katibu Mkuu wa PRST, Ndege Makura, akizungumza na waandshi wa habari.

 

Mwanachama wa PRST ambaye pia ni Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara, akizungumza katika mkutano huo.

 

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Chama cha Maafisa Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST) kimewakumbusha na kuwataka maafisa uhusiano nchini kufanya kazi kwa kutekeleza majukumu yao kwa niaba ya taasisi zilizowaajiri na sio watu wanaongoza taasisi hizo.

Aidha, chama hicho kimewaomba wanahabari kuwasilisha changamoto wanazokutana nazo kutoka kwa maafisa uhusiano kwa ajili ya kufanyiwa utatuzi kwani PRST lengo likiwa kuendeleza uhusiano uliopo.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa PRST, Ndege Makura katika Mkutano Mkuu wa Chama hicho uliofanyika jijini humo.

Amesema kuwa kumekuwapo na baadhi ya maafisa hao wanaosahau majukumu wanaotakiwa kuyafanya ndani ya taasisi wanazofanyia kazi kwani hufanya kazi ya kuwatangaza watu badala ya kufanya kazi kwa niaba ya taasisi zao.

" Mbrand taasisi sio watu tuhakikishe tunajikita kufanya kazi kwa niaba ya taasisi si vinginevyo maafisa uhusiano wanatakiwa kutambua majukumu yao ndani ya taasisi," amesema Makura.

Amebainisha kuwa wanahabari na wanachama kuendeleza uhusiano mzuri  na kwamba endapo kutatokea changamoto wasisite kuziwasilisha mbele ya chama hicho kwa utatuzi.

Amesisitiza kuwa wanahabari na PRST ni vyombo vinavyotegemeana hivyo hakuna haja ya kukosana na kwamba changamoto zinapotokea wazipeleke kwenye chama hicho.

Ameongeza kuwa chama hicho kina wanachama 364 waliopo kazini huku wengine wakiwa katika Vyuo Vikuu nchini kikiwemo cha Mtakatifu Augustine, Mwanza, Chuo cha Usafirishaji Tanzania (NIT) na Chuo Kikuu cha Tumaini- Tawi la Dar es Salaam (TUDARCO).

Amefafanua kuwa katika mkutano huo umekikutanisha chama hicho na wadau kutoka Serikalin na sekta binafsi na kwamba wamejadili mambo mbalimbali yaliyojikita kukuza taaluma hiyo.

Kwa upande wake, Mwanachama wa PRST ambaye pia ni Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amesema kupitia mkutano amejifunza mambo mengi ikiwemo wajibu wake katika taaluma ya afisa uhusiano.  


No comments:

Post a Comment

Pages