MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Buruhani Nyenzi, ameiagiza mamlaka hiyo kusimamia sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania namba 2/2019 kikamilifu.
Amezungumza hayo wakati akifungua rasmi Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), lililofanyika mkoani Morogoro leo Novemba 29,2021.
“Nawaagiza mkasimamie sheria hii kikamilifu ikiwa ni pamoja na ukusanyaji wa mapato katika maeneo yaliyoainishwa. Hii itasaidia kuwezesha utekelezaji wa majukumu yenu kwa ufanisi mkubwa pamoja na kutatua changamoto mbali mbali zilizo katika uwezo wenu.
“Nimejulishwa pia kuwa ili kutekeleza sheria iliyoanzisha taasisi hii mmefanikiwa kuandaa kanuni zitakazowezesha utekelezaji wa sheria hiyo.
“...Katika eneo hili, niwapongeze kwa kukamilisha kanuni saba za Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, ikiwemo Kanuni ya Tozo.
Natambua kuwa kanuni hizi zimeshasainiwa, kilichobaki ni utekelezaji wake tu,” anasisitiza Dk. Nyenzi.
Pia aliipongeza TMA kwa kazi nzuri inayofanyika na kuwataka kuchapa kazi kwa bidii na kuendelea kutoa taarifa kwa watoa maamuzi ili kusaidia ufanyaji wa maamuzi na kuwezesha serikali kukabiliana na changamoto zinazosababishwa na matukio ya hali mbaya ya hewa ambayo yanazidi kuongezeka kutokana na mabadiliko ya tabianchi.
Akizungumzia ushiriki wa TMA katika mkutano mkubwa wa COP26 ambao Rais Mama Samia Suluhu Hassan, alishiriki na kuhutubia mkutano huo.
Alisema, anatambua katika maazimio ya mkutano huo TMA inajukumu la kufanya ili kufanikisha jitihada za kuhimili athari za mabadiliko ya tabia nchi, hivyo, jukumu hilo litatimizwa vyema kwani TMA ina wataalamu wanaokubalika kimataifa wakiwemo wajumbe katika kamati mbali mbali za Shirika la Hali ya Hewa Duniani na Mwenyekiti wa Baraza hili ambaye ni Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO),” alibainisha Dk. Nyenzi.
B
Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dk. Nyezi.
Dk. Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TMA.
Baadhi ya wafanyakazi wa TMA.
No comments:
Post a Comment