Miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa nchi nzima imeleta neema na unafuu mkubwa kwa jamii.
Hayo
yamebainishwa na Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu wakati
alipofanya ziara ya kawaida ya ukaguzi wa miradi wa maendeleo ya Elimu
ya ustawi wa jamii kwa Taifa dhidi ya mapambano ya Uviko 19 ambapo
amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan kwa kuleta neema kubwa kwa Watanzania kupitia miradi hiyo.
"Miradi
hii ya Elimu si tu inaenda kupunguza tatizo la uhaba wa vyumba vya
madarasa bali pia inawaimarisha Wananchi kiuchumi. Mathalani kuna
Mafundi viongozi na Masaidia wamepata kazi za ujenzi,wanaingiza fedha;
Kuna Wafanyabiashara, Wasafirishaji, Wauzaji vifaa vya ujenzi madukani,
Wauzaji vifaa vya kujengea kama vile mawe, kokoto, mchanga nk hawa wote
wamepata neema ama fursa ya kufanya biashara, kujiongezea kipato kupitia
utekelezaji ujenzi miradi hii ya Elimu na mengineyo. Hivyo kwa niaba ya
Wananchi wa Tarafa ya Mihambwe tunamshukuru sana Rais Samia kwa miradi
hii inayoenda kuondoa uhaba wa Madarasa na pia amefanya mzunguko wa
fedha uongezeke kwa jamii ambapo miradi hiyo inatekelezwa." Alisema
Gavana Shilatu.
Gavana
Shilatu pia alitumia ziara hiyo kuwasisitiza Mafundi kuongeza kasi zaidi
ya ujenzi, kamati za miradi kuhakikisha wanasimamia ubora wa vifaa na
ujenzi ili miradi ikamilike kwa wakati, kwa ubora unaolingana na thamani
ya fedha.
Tarafa ya
Mihambwe imepata fedha toka Serikali kuu Tsh. Milioni 420 kujenga vyumba
vya Madarasa 19 kwa shule za Sekondari 5 na vyumba Madarasa 2 kwa
shule Shikizi moja. Katika fedha hizo hizo pia wanajenga ofisi 9 za
Waalimu na kuweka viti na meza kwenye Madarasa hayo yote 21.
No comments:
Post a Comment