NA MIRAJI MSALA, DAR ES SALAAM
Shirika la Omuka Hub iliyoanzishwa na Mhe Neema Lugangira kwa lengo la kuimarisha ushiriki wa sekta ya kidijitali kwa vijana, wanawake, wanahabri, shule na usalama wa intaneti kwa mikoa iliyo pembezoni mwa Tanzania.
Moja ya Vipaumbele vya Omuka Hub ni kuhakikisha kunawepo mazingira wezeshi ya kuwafanya Wanawake Wanasiasa kuwa salama wanapokuwa Mitandaoni hivyo kuanzisha Programu ya Kupinga Ukatilii wa Kijinsia Mitandaoni kwa Wanawake Wanasiasa.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Omuka Hub, Lovelet Lwakatare, wakati wa Maonyesho ya Zana za Kidigitali ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
“Kwa upande wa Ukatili wa Kijinsia, sisi Omuka Hub tumejikita zaidi katika kupambana na ukatili wa kijinsia mitandaoni wanaofanyiwa wanawake wanasiasa na kupitia programu yetu hii tumeanzisha Kikundi cha Wabunge Vinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake Wanasiasa. Kikundi hiki kina Wabunge 21 vinara kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao wanatusaidia kupaza sauti kupinga ukatili wa aina hii na tutashirikiana katika kuhakikisha tunaweza mazingira wezeshi ya usalama mitandaoni kupitia maboresho wa Sera, Sheria na Kanuni.” Alisema Lovelet.
Wabunge 21 ambao ni Wabunge Vinara wa Kupinga Ukatilii wa Kijinsia Mitandaoni kwa Wanawake Wanasiasa (MP Champions Addressing Online Gender Based Violence on Women in Politics) ni
1. Mhe Neema Lugangira
2. Mhe Salome Makamba
3. Mhe Nusrat Hanje
4. Mhe Judith Kapinga
5. Mhe Felista Njau
6. Mhe Condester Sichalwe
7. Mhe Ng'wasi Kamani
8. Mhe Jessica Kishoa
9. Mhe Keysha Khadija Taya
10. Mhe Tauhida Garlos
11. Mhe Mariam Ditopile
12. Mhe Catherine Magige
13. Mhe Lathifa Juakali
14. Mhe Rashid Shangazi
15. Mhe Elly Kingu
16. Mhe Abubakari Assenga
17. Mhe Festo Sanga
18. Mhe Rama S. Rama
19. Mhe Zaytuni Swai
20. Mhe Kassim Haji
21. Mhe Jacqueline Msongozi
Aidha aliongeza kuwa uzoefu mitandaoni unatuonyesha kwamba wanawake wanasiasa wanavyokuwa katika mitandao ya kijamii na wakiweka kazi zao, kuna idadi kubwa ya watu ambao hawajikiti katika hoja kwa kuchangia au kuuliza maswali bali wanahamishia hoja upande wa uanamke wao kama muonekano wao, jambo ambalo halifanyiki kwa wanaume wanasiasa.
"Shirika la Omuka Hub inapinga ukatili huo na tunataka tuchangie kuweka usawa wa kijinsia mitandaoni ili mwanamke mwanasiasa aweze kutumia Mitandao kwa uhuru sawa na makundi mengine. Hii itasaidia wanawake waweze kujiamini wanapokuwa katika mitandao ya kijamii kuzungumza na wananchi wao bila kuulizwa kwa nini nywele amekata, kwanini amevaa vile ambavyo amevaa, anafaa kwa hili, kwa lile na hivyo ndivyo ambavyo tutawawezesha wanawake wengi zaidi kushiriki kwenye siasa na kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa.
Katika maadhimisho hayo ya siku 16 kupinga ukatili wa kijinsia duniani kote ambayo dunia inajitambulisha kama The ‘Orange World’ “Sisi Omuka Hub tunapinga, tunakemea tunatoa rai kwa watu wote kuacha ukatili wa kijinsia wanaofanya mitandaoni kwa wanawake wanasiasa na tunahamasisha watu wanapokuwa katika mijadala waweze kuchangia kwa hoja na isiwe muonekano wao, mavazi yao, familia zao au masuala yao binafsi." Alisema Lovelet.
"Kwa niaba ya Omuka Hub tunamshukuru sana Madam Geline Fuko, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tangible Tanzania kwa kutupa fursa ya kuwa kati ya Mashirika yaliyochaguliwa kushiriki katika maonyesho ya teknologia ya kupambana na ukatili wa kijinsia katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam, tarehe 26 Novemba 2021" alimalizia Lovelet.
No comments:
Post a Comment