Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Macrice Mbodo akifafanua jambo katika mkutano na wanahabari wakati wa hafla fupi ya kumtambulisha Balozi wa Posta, Mshahiri Mrisho Mpoto (kushoto), iliyofanyika leo Dar es Salaam.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Shirika la Posta Tanzania limeingia makubaliano ya pamoja na Msanii wa nyimbo za asili na mashairi kuwa Balozi wa kulitangaza na kutangaza huduma na bidhaa za shirika hilo ambalo lipo katika mabadiliko ya kiteknolojia katika utoaji huduma zake.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam katika hafla hiyo iliyoambatana na utiaji saini makubaliano hayo Posta Masta Mkuu Macrice Mbodo amesema wameamua kumpa ubalozi msanii huyo lengo likiwa kutangaza mabadiliko na mageuzi yanayoendelea kufanyika kufahamika kwa wananchi ikiwemo utoaji wa huduma kwa njia za kidijitali pamoja uboreshaji wa miundo mbinu ya usafirishaji.
" Tumeamua kumpa ubalozi Mpoto sababu tunataka mabadiliko na mageuzi yanayoendelea ndani ya shirika yafahamike na Watanzania Posta ya leo ni ya kidijitali imeboreshwa kuanzia utoaji huduma hata miundo mbinu ya usafirishaji," amesema Mbodo.
Mbodo amebainisha kuwa kupitia Msanii Mpoto wananchi watafahamu fursa nyingi zinazopatikana Posta ikiwemo huduma ya duka mtandao ambayo humwezesha mteja kuuza na kununua bidhaa kwa njia ya mtandao duniani, huduma za usafirishaji wa dagaa na samaki nje yanchi, hiduma za kifedha zinazotolewa katika shirika hilo na huduma za pamoja zinazopatikana katika ofisi zote za Posta nchi nzima.
Amesisitiza kuwa kutokana na shirika hilo kufanya mabadiliko na maboresho ya huduma za limeweza kutambulika na kuheshimika Afrika hivyo hivi wanategemea kupata ugeni kutoka Shirikisho la Posta Duniani.
Ametoa wito kwa Watanzania kuthamini shirika lao la Posta kwa kutumia huduma zake kama mataifa mengine yanavyothamini mashirika yao ya posta ikiwemo Shirika la DHL la Ujerumani na Royal Mail la Uingereza lililowashirikisha kusafirisha Kifimbo ca Malkia hadi hapa nchini.
Kwa upande wake, Balozi Mpoto, amelishukuru shirika hilo kwa kumwamini na kumpa ubalozi na kuwasisitiza watanzania kutahmini vitu vyao ili waheshimike na mataifa mengine.
Mpoto amesema atautumia vyema ubalozi wake kuifahamisha jamii huduma zinazotolewa zikiwemo huduma za pamoja ambapo mteja anapatiwa huduma za BRELA, NIDA, RITA, TRA ,Uhamiaji, huduma za kifedha na duka mtandao.
No comments:
Post a Comment