Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Francis Nanai akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika Uzinduzi wa Mradi wa kukuza Chapa za wafanyabiashara wadogo kuwa kubwa na kuziuza duniani.
Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Mwajuma Hamza akizungumza kuhusiana na wanawake wafanyabiashara kuchangamki fursa za Mradi wa AfRAP katika uzinduzi wake jijini Dar es Salaam leo.
Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
TAASISI
ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imepata msaada wa zaidi ya dola Milioni 700
kwa ajili ya Mradi wa Kukuza na kuendeleza wafanyabiashara wadogo kukua
na chapa zao na kuuza duniani kote.
Msaada
huo ni kutoka Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) ambapo Tanzania kwa nchi
za Afrika Mashariki ndio ya kwanza kuwa na Mradi huo unaojulikana kama
Africa Franchising Accelerator (AFRAP) 2021-2025.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es Salaam katika Uzinduzi wa mradi huo na
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Francis Nanai ambapo amesema mradi
utazalisha ajira za moja kwa moja 38,000 na zile zisizo moja kwa moja ni
ajira 56,000.
Amebainisha
kuwa wafanyabiashara wa wakikuza chapa na kuuza duniani kote
watasaidia katika ukuaji wa uchumi na kufanya nchi kuwa imara kiuchumi.
Mkurugenzi
huyo amesema kuwa baadhi ya kampuni ambazo zilianza ukuaji huo ni
Pepsi, Coca Cola, KFC ambazo Chapa zake zilikuwa zinauzwa na kueneaa
Duniani hali ambayo wafanyabiashara wadogo wanaanza kujengwa kufika
huko.
Amesisitiza
kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amefungua Uchumi wa Nchi hivyo ni kazi ya
watanzania kuchangamkia fursa hiyo ambapo TPSF ipo kwa ajili ya kuona
biashara zinakua kwa kasi.
Nanai
ameongeza kuwa vigezo vya kuingia kwa wafanyabiashara wadogo kwanza ni
kuwa na leseni za biashara ,kampuni zao ziwe zimekaguliwa mahesabu kwa
miaka mitatu mfululizo,Mauzo ya Biashara kwa mwaka sh.milioni 250 pamoja
na ulipaji kodi katika mifumo iliyowekwa na nchi.
Amefafanua
kuwa mradi utachukua miezi 48 ambapo wataanza na mafunzo visiwani
Zanzibar kuanzia Novemba 22 mwaka huu na kwenda Jijini Mwanza ,Mbeya na
mikoa mingine huku Dar es Salaam itapata mafunzo mwakani.
"Mradi
huu haufanywi kihuni huni ndio maana vigezo hivyo ni kwa ajili ya
kupata washindani ambao wana uwezo wa kukuza chapa zao na Taifa kuwa na
wafanyabiashara wenye chapa zao kuzunguka ulimwenguni,"amesema Nanai.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake
Tanzania (TWCC) Mwajuma Hamza amesema kuwa wanategemea wanawake asilimia
50 wataingia katika mradi huo na kuinuka na chapa zao.
Nae,
Mshauri wa Mradi wa AFRAP Wambugu wa Gichohi amesema kuwa mradi huo
umekuja kuinua biashara kwa kukuza chapa 'Brand' na kuingia katika
ushindani wa masoko nje Tanzania.
No comments:
Post a Comment