HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 17, 2021

Dk. Kahesa : Tatitzo la Saratani ya matiti litaongezeka siku zijazo ikilinganishwa na miaka 10 iliyopita


Mkurugenzi wa Huduma za Kinga ya Saratani kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Dk. Crispin Kahesa.

 

Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam

SARATANI (Cancer), ni jina la kibantu lakini kwa wengi wanafahamu kama Cancer.

Kuna aina zaidi ya 200 za ugonjwa wa Saratani ikiwamo ya matiti  na hutajwa kulingana na eneo gani la kiungo ambacho kimeathiriwa mfano Saratani ya titi ni kutokana na eneo lilioathiriwa.

Pia Saratani ya matiti inaathiri makundi yote akina mama na akina baba na asilimia 99 ya wahanga ni akina mama  na akina baba ni asilimia moja tu.

Asilimia moja ya akina baba inatokana na sababu mbalimbali zikiwamo za kimaumbile na kibaiolojia kama aina ya vichocheo vua mwili na aina ya titi lililopo na ufanyaji kazi wake.

Akizungumza  katika mahojiano na gazeti hilo ofisini kwake Mkurugenzi wa Huduma za Kinga ya Saratani kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Dk. Crispin Kahesa anasema kutokana na hali iliyopo kwa sasa inaonyesha siku zijazo tatizo la ugonjwa huo  litaongezeka.

Dk. Kahesa anasema kuwa Saratani ya matiti kwa akina mama inashika nafasi ya pili hapa nchini na ulimwenguni satarani hiyo inaongezeka.

Anasema kwa hapa Tanzania inachukua asilimia 16 kati ya wagonjwa wanaofika katika Taasisi hiyo 16 wana Saratani ya matiti.

" Hapa Ocean Road tunawaona wagonjwa wapya 5200 kila mwaka kati ya hao wagonjwa zaidi ya 800   kwa takwimu za mwaka jana" anaongeza.

Hali tunayoiona kwa sasa ikilinganishwa na miaka 10 iliyopita ugonjwa wa Saratani ulikuwa unachukua nafasi ya sita  lakini kwa sasa unachukua nafasi ya pili, " anasema Dk Kahesa.

Anaeleza kuwa hali hiyo inatokana na mabadiliko ya mfumo wa maisha na kwamba kibaya zaidi umri wa waathirika umeanza kushuka zaidi ya miaka 6 kuliko miaka iliyopita.

Dk. Kahesa anafafanua kuwa ugonjwa huo unatokea mapema kwa jamii, watu wameanza kuishi mfumo ambao si asili katika  umri mdogo  wakati mwingine inawezekana hata vizazi vinapata kemikali kama vile zinazotokana na tumbaku kutoka kwa wazazi wao .

Anasema kutokana ma kemikali hizo ni rahisi ugonjwa kuanza kutokea kwa watoto hao

WAATHIRIKA

DK.Kahesa anasema huo ni ugonjwa ambao unawakuta watu wazima waliopevuka na umri wa chini ni maika 25 na kuendelea.

" Wastani wa umari wa waathirika  wakubwa kwa upande wa nchi za Afrika ni kuanzia miaka 54 , umri huo pia unaendelea kushuka kwa sababu ya mwamumko na nnwitikio  umekuwa  ni mkubwa watu wanawahi kufika Hospitali," anasema.

Anaongeza kuwa kipindi cha nyuma  walikuwa wanawaona watu wa umri  wa miaka 60  na ugonjwa ulikuwa katika hatua ya tatu na ya nne.

Mkurugenzi huyo wa Huduma za Kinga anasema mtu alikuwa akionekana ameathirika kwa muda mrefu  lakini anachelewa kufika hospitali.

Anasema kwa sasa wastani umeshuka wameanza kuona ugonjwa ukiwa katika hatua za chini kabisa.

SABABU

DK. Kahesa anabainisha kuwa  Saratani inatokea kutokana na visababishi au vichochezi hatarishi amavyo vimegawanyika katika makundi manne.

Anafafanua kuwa kuni la kwanza ni suala la jinsia mwanamke ana hatari mara 10 zaidi ya nwanaume.

Dk.Kahesa anaeleza kwamba umri pia unavyozidi kuongezeka hatari ya mtu kupata Saratani inaongezeka.

"Huwezi kuona Saratani hii katika umri mdogo na huwezi kukuta mtoto ana Saratani ya matiti," anaeleza.

Anaongeza kuwa sababu nyingine ni kemikali hatarishi amabazo zinegawanyika katika makundi tofauti tofauti zinazopatika kwenye matumizi ya sigara , tumbaku  na zile zinazopatikana
viwandani.

" Kuna sababu nyingine za kibaiolojia kwani Kuna vichocheo vya mwili yaani homoni, Kuna baadhi ya vyakula vikitumiwa kwa matumizi ambayo sio sahihi vinasababisha kuongezeka kwa baadhi ya vichocheo hasa vyakula vyenye mafuta vimeonekana kuongeza vichocheo," anasema DK.Kahesa.

Anasema ukosefu wa mazoezi unasababisha kuratibu vichocheo ndio maana akina mama wanaathirika zaidi kuliko wanaume.

KURITHI

Mkurugenzi huyo wa Huduma za Kinga anaeleza kuwa kuna baadhi ya watu kwenye makundi ya jamii wanahatari kubwa kuliko wengine  katika  familia zao wanapata Saratani ya kurithi.

Anasema  inategemea aina ya tamaduni za familia  vyakula wanavyokula na wengine labda Wana aina ya vinasaba vya kurithi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine .

DK.Kahesa anabainisha kuwa ukosefu wa baadhi ya aina za vyakula ambavyo vinazuia Saratani kama vile mboga za majani jamii ya matunda hivyo vyote zinazuia Saratani hiyo.

Anaeleza vyakula vinavyoogoza kusababisha Saratani ni vya mafuta kama vile vyama na vyenye kimikali na vitu vya Viwandani.

Dk. Kahesa anasema vichocheo hivyo vinasababisha mwili kuongeza chembe chembe hai zinazo kua bila mpangilio amabazo zinaweza kubadilika na kuwa saratani.

DALILI ZAKE

Anasema katika hatua za awali watu hawagundui dalili labda kwa vipimo maalumu kwa sababu mabadiliko hayo yanakuwa ni ya ndani ambayo yapo kwenye chembe hai.

" Wengi wanakuja kuona dalili pale chembe chembe hai zinapogeuka kuwa saratani zinakua bila mpangilio.Dalili zinazoonekana ni kutokana na kuwa na uvimbe kwenye titi," anasema.

Anasema wengine wanapata maumivu kwenye titi na hiyo inatokana na uvimbe huo kubonyeza baadhi ya mishipa ya fahamu.

Dk. Kahesa anasema dalili nyingine ni kuona uzito wa titi moja kuliko jingine na wakati mwingine chuchu zinaanza kutoa maji yenye rangi au damu.

" Uvimbe unavyoendelea kukua baadae unaweza kubadilika ukawa kidonda au muonekana wa titi ukabadilika. Chichu zinabadilika ganda la juu linaweza kuwa kama limao chuchu inaingia ndani," anasema.

Anasema watu wengi wanaowaona katika taasisi hiyo ni wale ambao wanasikia maumivu kwenye titi unaosababisha mitoki kwenye kwapa  na baadhi yao kuwa na vidonda.

No comments:

Post a Comment

Pages